Msaada: Mtoto wa darasa la nne ana kesi ya kulawiti watoto wenzake, ni hatua gani huchukuliwa kisheria kumuwajibisha?

Msaada: Mtoto wa darasa la nne ana kesi ya kulawiti watoto wenzake, ni hatua gani huchukuliwa kisheria kumuwajibisha?

Atapelekwa jela ya watoto akithibitika tuhuma zinazomkabili
Ndo nataka kujua maana yupo darasa la 4 kwaiyo akihukumiwa miaka 30 kwaiyo magereza wataweza kumtunza kuanzia darasa la 4 au kuna hukumu tofauti na iyo
 
Ndo nataka kujua maana yupo darasa la 4 kwaiyo akihukumiwa miaka 30 kwaiyo magereza wataweza kumtunza kuanzia darasa la 4 au kuna hukumu tofauti na iyo
Kuna mahakama za watoto faili lake litapelekwa huko ikithibitika andaa maandalizi ya nauli kwenda kumsalimia hadi amalize kifungo

Simamieni mienendo ya watoto
 
Ndo nataka kujua maana yupo darasa la 4 kwaiyo akihukumiwa miaka 30 kwaiyo magereza wataweza kumtunza kuanzia darasa la 4 au kuna hukumu tofauti na iyo
Mtoto Kuwa darsa la 4 sio sababu ya kutokuhukumiwa. Sheria itachukua Mkondo wake.
 
Aisee! Mwenyezi Mungu alinde vizazi vyetu. Kuna kitu hakiko sawa kwenye Ulimwengu wa roho.

Hapo correction facilities zitafanya kazi yake.
 
Ukisoma vifungu vya Sheria zimeanzia kwa watu wenye umri wa miaka 18 Ila wenye ufahamu watakuelewesha zaidi
Naamini watazingatia kwamba zipo Haki za mtoto. Kama zipo Haki za Mtoto ni lazima pia kuwepo Wajibu wa mtoto. Kwa mantiki hiyo; Kama kuna Haki na Wajibu ni lazima Ziwepo Sheria zinazolinda haki na wajibu huo. Je, kama mtoto hatimizi wajibu wake itakuwaje? Je, Kama mtoto mmoja anavunja Haki za watoto wenzake itakuwaje? Ukiangalia hoja hizo kwa mapana yake utaona ni lazima ziwepo sheria za kumwajibisha mtoto mtundu, mtoto mfidhuli au mtoto mkorofi kama huyo anayewalawiti watoto wenzake. Huyo ni mtoto mkosaji.
NB: Soma Sheria za watoto za mwaka 2014, sura ya 13 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Wazazi wengi tumesahau malezi
Yeah. Lakini linapokuja suala la mtoto kutenda kosa la kijinai e.g. Kulawiti watoto wenzake; Wazazi/Walezi wanaweza kuwajibishwa kwa kosa la kuzembea malezi ya mtoto wao.
 
Back
Top Bottom