Msaada !! Mtoto wangu shingo yake haijakaza na anangalia upande mmoja sanaaa

tingiga

New Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
1
Reaction score
2
Helloo Guyz

Habarini jamani

Naombaa msaadaaa mwenye mawazo juu ya Mwanangu.Mtoto wangu ana miezi sita ni mchangamfu sana ila shida yake ni shingo yake bado haijakaza vizuri kabisa na anaangalia upande mmoja sana.Baada ya kuona hilo nimempeleka hosipitali daktari akaniambia kwamba ana tatizo la "Neck Palse". Mama yake alimbana shingo wakati wa kujifungua. Nimeambiwa niende hospital ya rufaa. Naombeni msaada wa kimawazo kumsaidia mwanangu aweze kupona jamanii. Asanteni sana.
 
Ndugu kesi hii nakushauri uiwasilishe Hospitali mapema kesho kabla shingo haijakakamaa, humu utageiwa matango pori maana kila mtu humu daktari
 
pole sana mkuu. mpeleke CCBRT wamchunguze, I hope atapata msaada unaostahili.
 
Ndugu kesi hii nakushauri uiwasilishe Hospitali mapema kesho kabla shingo haijakakamaa, humu utageiwa matango pori maana kila mtu humu daktari

kaleta humu anajua kuwa atapata msaada wa mawazo,kumbuka mwili sio gari useme fanya hivi litatembea. hata vyuoni madaktari wamefundishwa ethics ni marufuku kutibu namna hii. ni lazima mgonjwa umuone upate historia yake ya ugonjwa,umfanyie examination ndio ujue tatizo sasa humu jf utamfanyia vp mgonjwa examination,cha msingi kwa sababu ni mtoto mdogo inabidi apelekwe kwa daktari wa watoto ili aweze kumsaidia
 
ufikishe kwa hospitali, wakati huohuo mfanyishe mazoezi ya kuangalia mbele,unamuweka kwenye beseni, unamzungushia nguo/khanga nyuma, kulia na kushoto kwa shingo ili yeye aangalie mbele tu.
uchunguzi ni muhimu.
 
Sijakataa,je anawezaje kutambua na kuchagua ushauri upi unafaa ikiwa kila mmoja atakuja na wazo lake hapa, ndio maana nimemshauri aende Hospitali kule atakutana na wataalam wa afya ya mtoto watamsaidia, zingatia afya haifanyiwi majaribio ndugu
 
Mambo vip ndugu ,hili tatizo la mwanao ulifanikiwa kupata msaada? mana mwanangu nae ana miezi 6 lakini shingo yake imekaa upande,ila ni mchangamfu kawaida ila tatizo nishingo kama imeegamia upande mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…