Msaada: Mtoto wangu wa kike miaka 3 ana UTI ya kujirudia rudia, tumetumia dawa nyingi na njia mbalimbali lakini tatizo haliishi

Msaada: Mtoto wangu wa kike miaka 3 ana UTI ya kujirudia rudia, tumetumia dawa nyingi na njia mbalimbali lakini tatizo haliishi

Wakuu karibuni,

Yaani hapa ninapoandika amekutwa tena ya Uti baada ya kumaliza dawa wiki iliyopita ya kutibu uti hio hio.

Pia soma: Je, UTI ni ugonjwa wa ngono?
Tafuta mlonge has mizizi yake!chemsha fungu moja Kwa Lita Moja na nusu ya maji,chemsha Hadi iive kabisa!

Mpoozeee halafu awe anakunywa Kwa chai vikombe viwili asubuhi na jioni!atakunywa maji na kukojoa sana!Hadi UTI itaisha!
 
Usafi, dada wa kazi anamtumbukiza kwenye beseni la maji kumwogesha, amsafishe huko chini kwanza.

Pampas anakaa nalo usiku kucha lenye mikojo na haja kubwa.

House gel ni mchafu mikono ikiwa michafu anamsafisha mtoto.

Unless otherwise dawa zinakuwa zime expire.

Kumpima wiki baada ya kumaliza dozi ni muda mfupi mno, pengine dawa bado zinafanya kazi.

Mwisho, kila njia kama iko sawa, simamia achome sindano.
 
Wakuu karibuni,

Yaani hapa ninapoandika amekutwa tena ya Uti baada ya kumaliza dawa wiki iliyopita ya kutibu uti hio hio.

Pia soma: Je, UTI ni ugonjwa wa ngono?

Ugonjwa waUTI(Urinary Tract Infection) siyo ugonjwa wa ngono. Hii inatokana na kwamba wadudu/bakteria/virusi wanaosababisha UTI hawana uwezo(adapted) kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia tajwa.

UTI nyingi ni za kujiambukiza hasa kwa wanawake kutokana na changamoto ya kimaumbile. Changamoto hii pia inaweza kuchochea suala hili kutokea wakati wa ngono, laki si njia rasmi ya maambukizi.

Wadudu/bakteria/virusi wanaoweza kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwinginekwa njia yango huwekwa kwenye kundi la ugonjwa wa STI(Sexual Transimitted Infection).

TIBA KWA UTI
1: Unapopatikana na UTI ni vyema kutumia dawa uliyopewa kwa kadri ya maelekezona kumaliza dozi. Unapomaliza dozi ni vyema kupima naafa ya siku mbili au tatu kuona kama umepona au la. Kama haujapona ni vyema KUOTESHA mkojo husika na kutibu kadri ya majibu husika. Kama huduma husika haipatikani, unuzi unaonyesha dawa ambazo hazitumiki mara kwa mara hufanya vyema zaidi(kuna dawa hazitumiki sana na jamii kwa sasa kutokana na uwepo wa dawa mpya).

2: Kwa watoto, hasa wa kike: Kuhakikisha usafi wa nguo zao za ndani, kutokuwaacha na mkojo au choo kikubwa kwa muda mrefu na kuwafanyia usafi mara tu wanapokuwa wamejisaidia.

3: Kutokutumia wipes zenye pombe/alcohol sehemu za siri. Huvuruga balansi ya aina ya bakteriakwenye njia ya uzazi.

KUHUSU UTI KUONGEZEKA KWENYE JAMII
Ni suala mtambuka, sababu ni nyingi kati ya hizo:
1: Ongezeko la vituo vya afya.
2: Uwepo wa teknolojia ya ugunduzi.
3: Mabadiliko kwenyemfumo wa maisha ie. Pampers
4: Ulaghai wa majibu/faida.
5: Uelewa wa utafsiri wa majibu/kutokuwa na elimu ya kutosha
6: Ongezeko la idadi ya watu.
7: Nk.
 
Usafi, dada wa kazi anamtumbukiza kwenye beseni la maji kumwogesha, amsafishe huko chini kwanza.

Pampas anakaa nalo usiku kucha lenye mikojo na haja kubwa.

House gel ni mchafu mikono ikiwa michafu anamsafisha mtoto.

Unless otherwise dawa zinakuwa zime expire.

Kumpima wiki baada ya kumaliza dozi ni muda mfupi mno, pengine dawa bado zinafanya kazi.

Mwisho, kila njia kama iko sawa, simamia achome sindano.
Mtoto wa miaka mitatu havai pampers jamani.... Wanawake tujitahidi hapa... Pampers mtoto aachishwe mapema iwezekanavyo... Utafurahi... 😅🙏🏾
 
Asipewe chips na fast foods.
Apewe matunda kwa wingi maji anywe yakutosha
 
Back
Top Bottom