Msaada muda wa kupokea documents DHL

Wikiliki

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
528
Reaction score
141
Wadau wa Jf nimeagiza gari kutoka japani na gari limeshafika Dar ila documents ambazo seller alinitumia kwa DHL hazijafika. Pia alinitumia tracking namba na nika track through website ya DHL nikaona parcel imepokelewa. Sasa ninaomba kuuliza huwa zinatumiaga siku ngapi kufika Dar. Asanteni.
 
Kwani yy hajakuambia zinatumia siku ngapi kufika? JF inafanya mijitu inakuwa milege lege, umeshindwa hata kuwapigia cm hao DHL kuwauliza ndg? Au unatangaza kua umenunua Vitz be forward?
 
Jibu swali mzee sio kuanza kulalamika. Wao wanasema hawana guarantee lini itafika.
 
DHL inachukua walau siku tatu kukufikia, na ikifika TZ DHL wanakukupigia simu wakafanya delivery hapo ulipo with extra charge..
 
DHL inachukua walau siku tatu kukufikia, na ikifika TZ DHL wanakukupigia simu wakafanya delivery hapo ulipo with extra charge..

DHL, UPS, FEDEX, EMS, TNT n.k. no Door to Door yaani wanaleta mpaka mlangoni kwako.., sasa sema tatizo la Bongo hakuna address ni vigumu wakuletee temeke jirani na Mangi karibia na mti wa Mwembe..., ndio maana uwa wanakupigia simu uifate ila kama wanaweza kufika ulipo na panaeleweka wanaleta mpaka mlangoni na ni jukumu lao..

Kuhusu mdau cheki kwenye tracking.., utakapoona received in Dar/Tanzania fahamu kwamba mzigo tayari wanao DHL, na kuepuka kufunga safari kuwafuata wapigie simu zao 255 22 2861000 / 4 kwa kawaida parcel kufika ni 4 to 5 working days.., na documents tu sio shida ingekuwa parcel ingechelewa sababu huwa wanangoja customs wacheki na wakadirie ushuru kabla ya kukutumia
 

Mkuu nenda DHL na hiyo track no. Watakushauri cha kufanys
 
Daaaah!! Pole maana doc zinafika wiki mbili yabla ya gar kufika Dar, ukichelewa ata gari hutolikuta.

system hacker wamekuibia hyo trucking number mkuu..
 
wadau wote ninawashukuru kwa ushauri wenu. Ni wa maana sana maana umenifungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…