Chanzo kilikuwa hivi, Team leader aliniandikia sms asubuh kuwa natakiwa kuingia kazin night,wakat iyo siku kawaida Mimi huwa nakuwa off, ilikuwa jumatatu na mtu anaeingiaga night iyo juma tatu yupo na hakuwa na excuse kwa maana ya ugonjwa au emergency yeyote maana mi nilimpigia simu uyo mwenzangu akathibitisha hilo kuwa hakuwa na tatitzo,
Kumbe Team leader anasema alikaa kikao siku ya jumamosi na kubadili ratiba ya kazi,watu waliokuwepo kwenye hichi kikao wanasema hakusema kitu kama hicho,na hata tulipokuwa hearing nilipomtaka athibitishe hilo alishindwa, kwa iyo alibadili ratiba kwa utashi wake na bila kutupa taarifa,sasa siku ya shift yangu ilipofika ilkuwa jumatano,ndipo aliponitaka niandike maelezo kwa nini sikufika kazini iyo siku ya jumatatu,akaamua kulipeleka suala juu kwa production manager,
nikaitwa nikaeleza kama nilivoeleza hapo juu,boss akatupilia mbali hilo kosa na akamtaka hilo suala lihishe na tufanye kazi kama kawaida,kumbe Team leader ule uamuzi haukumridhisha ili hali alikubali yahishe mveke ya boss,ndipo alipoamua kwenda HR ofisi kushitaki,huko sasa nikaitwe,ile kufika tu uyo afisa mwajiri akaanga kama kunihukumu bila kunisikiliza,ina maana aliona yule Team leader yupo sahihi,aliniuliza maswaki kama,"iv utajisikiaje watu wakisema umekuwa terminated?
Hapo hata hajanisikiliza bado, nilipoomba nafasi ya kujieleza hakunipa,binafsi nilikereka nikaamua kuondoka nikawaacha wenyewe maana niliona hakuna haki pale, ndipo nikaitwa hearing,sasa hearing suala la kutofika kazini waliniona nimeonewa ivo wakaniambia sina hatia, sasa walinikuta na hatia kosa la pili hilo la kuondoka kwa uyo afisa mwajiri,na kukataa kuandika maelezo.