Msaada: Mwanangu anasumbuliwa na majipu

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Posts
8,328
Reaction score
7,784
Wakuu naombeni msaada, mtoto wa kaka yangu ana mwaka na nusu lakini kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na majipu sehemu mbali mbali za mwili wake. Tushampeleka hospitals mbali mbali kwa maspeshalisti kadhaa bila mafanikio.

Tumempima allergy pia imetokea kuwa hana allergy ya kitu chochote.

Msaada tafadhali madoctor na msio madaktari.
 
MaSpecialists waliwaambia nini? Au walivyoona sio allergy wakasema basi rudi nyumbani?
 
Dr Liwa, Dr MziziMkavu msaada wenu

Pole sana. Ana umri gani huyo mtoto. jaribu hospitali zingine na utapata jibu. vifaa na ujuzi unatofautiana. kuna jamaa alikuwa na tatizo hilo pia. kama utashindwa huko nitafute nitakuunganisha nae akupe maelezo alichofanya kwa maelezo mtafute
0689417472
 
Kama hayamletei homa huyo hana tatizo lolote,ni hali ya hewa ya joto tu inamsumbua.

Hakikisha analala sehemu yenye feni (zaidi feni ya juu) au ac mda mwingi.
Hakikisha anashinda na kulala na nguo nyepesi kabisa.

Mtoto aogeshwe kabla ya kulala na akitoka kulala.
Nakuhakikishia tatizo litakua historia.


Mimi nae wangu alikua hivyo hivyo lkn baada ya kupata ushauri wa dokta mzuri tatizo liliisha kabisa.
 
Asante mkuu, nitampa namba muhusiia.
Anaelekea mwaka na nusu sasa.


Kuna wkati anapata homa mkuu, asante sana kwa ushauri mkuu
 
Ni mchafuko wa damu tu. Hii itamsaidia kwa baadae
 
Mpimeni na HIV pia.Kuna mtoto majibu yalikuwa hayamuishi mara kichwani na sehemu mbalimbali za mwili kumbe wazazi wake walimzaa wakiwa wameathirika na yeye akawa kaambukizwa
 
Tulisumbuliwa na tatizo hilo kwa muda...ila limeisha baada ya kupimwa na kukutwa alikuwa na UTI iliyokuwa imekaa muda mrefu...jaribuni
 
Hospitali yake huyu itakuwa pale mtaa wa Magogoni. Mpeleke tu pale atatibiwa na kupona mara moja mkuu.
 
Itamsaidia kivipi mkuu
Bado mdogo na anakua hivyo mwili unatabia ya kujenga immunity naturally... Kwa hiyo kwa hapo baadae akikua inshaalah mambo ya maradhi maradhi yanakua hayamsumbui... Ila majipu ni bacterial infection unaweza tumia antibiotics au tiba za asili kama maziwa, kitunguu etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…