Msaada,mwenge secondary-singida

JAK

Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
92
Reaction score
20
Kwa anayefahamu mahitaji ya shule tajwa naomba anisadie.
 
Ni shule kongwe imeanzishwa mwaka 1967, ipo singida mjini, ina kombi zisizopungua 8, PCB,HGL,EGM,HKL,CBG,HGE,PCM,HGK, huwezi kufaulu hata kwa dawa kama utategemea waalimu, kifupi ni shule yenye uhuru wa kila aina hivyo umakini mkubwa unahitajika kuweza kutimiza safari yako ya masomo,pia ina a level pekee yake, ni boys, nmesoma hapo
 
Rim A4 lazma,files , vngne counters ,pen ,penseli ,mafuta,sabuni,kiwi, calculator kama we unasoma sayansi au egm na hge,bukta ya blue ya michezo ,pair ya rubber za michezo,viatu black vya kamba,surual ya damu ya mzee mbili, surual ya kaki ya kushindia ya kuwaonyeshea tu baada ya hapo we utajiachia na vaz unalotaka,shat mbili nyeupe mikono mirefu, utaenda na pesa ya tai,sweta na tishet sikumbuk ni shngapi,....ila haizidi elfu50,pesa ya michango mbalimbali haizidi 130000, Ada kama kawa kwa muhula 35 elfu.
Gallon la kutunzia maji ya kunywa ni lazma litre tano,godoro 3x2 ,shuka za light blue mbili,blanket manake kuna baridi balaa,net,ndoo ya maji(ila ukifika watu wanashare sana ndoo chako changu changu chako) ,malapa,kuna vitu vingine utanunulia hapohapo mjini sababu shule ipo mjini kabisa.
na vngne nimesahau coz nimemalizapo this year.
Ile joining ndio ya muhimu sababu ina form ambazo mzazi na mkuu wa wilaya na mganga wanatakiwa wajaze na kusaini
Kwa maelezo mengne zaidi ni PM ntakusaidia namb za madogo wa pale niliowaacha.Thank u
 
Mwenge? Du. Nilisoma hapo miaka ya tisini mwishoni.

Enzi zetu A level ilikuwa PCB pekee na sare ilikuwa khaki. Shule ina mvuto, majengo safi. Tatizo walimu. Mie nilifundishwa na mmoja anaitwa Lali. Ha ha ha. Wacha kabisa. Kila siku akija topic mpya.

Usitishike. Jiandae kufanya mikesha ya kitaaluma. Ila ukishafaulu pale dogo, we jua umetoboa mpaka PhD. Mifano mingi. Mmoja ni kamanda wetu Kitila Mkumbo, Dean wa faculty ya Elimu DUCE.

Kila lililo jema. Nitakutembelea hapo mwakani nikiwa likizo.
 
Nimekusoma Mkuu
 
Pamoja mkuu, nitafuata nyayo za huyo mwanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…