MSAADA: Mwenye kujua taratibu za kumhamisha mtoto toka shule binafsi kurudi shule za serikali

NgerukeAbra

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
1,336
Reaction score
2,008
Amani ya bwana iwe juu yenu waungwana.

Kama kichwa cha habari kinavyojielezq,nina kijana wangu yupo kidato cha kwanza shule binafsi iliyopo Pongwe-Tanga,alihitimu elimu ya msingi Dar es salaam na kuchaguliwa kujiunga na shule ya serikali ya kata iliyopo maeneo ya Chanika.

Nilifuata taratibu zote za kumuhanisha na kumpeleka shule binafsi, kiukweli sasa 'vyuma vimekaza'' nataka nimrudishe tena shule za serikali.

Nimewauliza watu kama wanne wote wamenijibu haiwezekani tena kumrudisha mtoto shule za serikali na mmoja wao alisema alienda hadi kwa afisa elimu wilaya kwa shida kama yangu alikataliwa.

Tafadhali watu wenye kujua taratibu nisaidieni hali yangu mbaya sana kiuchumi watu wa TAMISEMI hapa jamii forum naombeni muongozo.
 
Amani ya bwana iwe juu yenu waungwana.

Kama kichwa cha habari kinavyojielezq,nina kijana wangu yupo kidato cha kwanza shule binafsi iliyopo Pongwe-Tanga,alihitimu elimu ya msingi Dar es salaam na kuchaguliwa kujiunga na shule ya serikali iitwayo Nguvu mpya ya Chanika.

Nilifuata taratibu zote za kumuhanisha na kumpeleka shule binafsi, kiukweli sasa 'vyuma vimekaza'' nataka nimrudishe tena shule za serikali.

Nimewauliza watu kama wanne wote wamenijibu haiwezekani tena kumrudisha mtoto shule za serikali na mmoja wao alisema alienda hadi kwa afisa elimu wilaya kwa shida kama yangu alikataliwa.

Tafadhali watu wenye kujua taratibu nisaidieni hali yangu mbaya sana kiuchumi watu wa TAMISEMI hapa jamii forum naombeni muongozo.
Mosi unatakiwa kuwa Mpole na urudi kinyonge kwenye shule ya serikali aliyochaguliwa, halfu ongea vizuri na mkuu wa shule... ikibidi mpige kwa kutumia hela... halfu uje utupe matokeo... inawezkna.. tatizo umetaja hadi shule.. ungeomba tu muongozo. Ila pambna
 
Hakutaja jina la shule mkuu, kasema maeneo ya chanika
 
Pole sana,haiwezekana Moja ya mambo muhimu magufuli alifanya ni mapoja kuhakikisha idara za nchi hii zinaingizwa tehama

Kama ingekuwa ni kabla ya mwezi wa 3 yaani Kabla ya midterm ingewezekana

Kwasababu wakuu wa shule zote hupeleka majina ya wanafunzi wizarani na kutoa sababu zakutolipoti ambao hawapo kwenye idadi ya wizara(hapa wizara inajua majina ya wanafunzi wote wanaopelekwa shule kata)

Ukitoa sababu yakuhama alienda wapi?

Shule za binafsi hivyohivyo mana wao ndo wanakuwa wamepokea Ile taarifa ya mtoto na wamekabidhi wizarani

Ngumu sana ,sahau

Chakukusaidia Kuna shule zipo na zinagharama ndogo ya karo....mfano kule mlimba ,pwani hapo gharama ni 1.5 Milion .....changamka
 
Mosi unatakiwa kuwa Mpole na urudi kinyonge kwenye shule ya serikali aliyochaguliwa, halfu ongea vizuri na mkuu wa shule... ikibidi mpige kwa kutumia hela... halfu uje utupe matokeo... inawezkna.. tatizo umetaja hadi shule.. ungeomba tu muongozo. Ila pambna
Mnaongea kiurahisi tu kwa kutumia uzoefu wa zamani, siku hizi Hali si shwari tena (ingawa simaanishi haiwezekani kwani mi ni mdogo sana kwenye hii Dunia). Siku hz kuna kitu kinaitwa PREM NUMBER (PREM #), hii ni namba ya utambulisho apewayo mtoto aanzapo shule ya msingi. Kila mtoto ana namba yake. Namba huhama na jina la mtoto kwenda kwenye shule yeyote anayoenda. Yaani, akipenda sekondari nayo huhamia huko sekondari na huondoka kabisa katika mfumo wa shule ya msingi aliyotoka. Hivyo hivyo, akimaliza sekondari (o'level) na kwenda advance Hali huwa hivyo hivyo, namba na jina vinatoka na kwenda huko advance anakoenda.

Kwenye kesi ya uhamisho ni hivyo hivyo; hakuna mkuu wa shule (labda kwa uzembe tu) atakayempokea mtoto kutoka shule nyingine bila hiyo PREM #. Wakuu wa private, kwa kufahamu kuwa mwanafunzi si wako bila PREM #, siku hizi wamejanjaruka na ndicho kitu muhimu kimojawapo wanachokuomba (ukiacha fedha, of course). Wakiipata tu na kumsajili mwanafunzi (mfumo unaruhusu) hapo anakuwa wao na hakuna shule yoyote (alizopita mtoto) ambako anabaki katika mfumo.

Kumtoa tena private kumpeleka serikalini, mtindio ni huo huo; prem # na mabadilishano ya kwenye mfumo. Mabadilishano haya ya kwenye mfumo Yana uhusika wa Moja kwa Moja wa maafisa elimu wilaya na mkoa. Hawa wanaona na wanajua aina ya shule zinazobadilishana wanafunzi (yaani za serikali, private au private na serikali). Kwakuwa utaratibu hauruhusu private kwenda serikali, kamwe hilo haliwezi kumalizwa na wakuu wa shule bila wilaya au mkoa kujua...... it's a big business, man!

Nawasilisha
 
Japo ni ngumu ila pambana utafanikiwa
 
Asante ndugu
 
Ni ngumu boss,Mimi nakushauri mhamishie private ya Bei ndogo kidogo,zipo nyingi tuu.
Na km dogo Ni kichwa Kuna baadhi ya private ambazo huwapunguzia Ada vipanga au kuwaondolea kabisa ili wapeperushe bendera za shule zao kwa matokeo bora.
 
Pole sana,haiwezekana Moja ya mambo muhimu magufuli alifanya ni mapoja kuhakikisha idara za nchi hii zinaingizwa tehama

Kama ingekuwa ni kabla ya mwezi wa 3 yaani Kabla ya midterm ingewezekana

Kwasababu wakuu wa shule zote hupeleka majina ya wanafunzi wizarani na kutoa sababu zakutolipoti ambao hawapo kwenye idadi ya wizara(hapa wizara inajua majina ya wanafunzi wote wanaopelekwa shule kata)

Ukitoa sababu yakuhama alienda wapi?

Shule za binafsi hivyohivyo mana wao ndo wanakuwa wamepokea Ile taarifa ya mtoto na wamekabidhi wizarani

Ngumu sana ,sahau

Chakukusaidia Kuna shule zipo na zinagharama ndogo ya karo....mfano kule mlimba ,pwani hapo gharama ni 1.5 Milion .....changamka
1.5 ndio pesa ndogo sio?
 
Back
Top Bottom