Msaada: Mwenye nyumba nimempa kodi kwa ajili ya kumalizia pango, ni muda umepita hajakamilisha ukarabati

Miracle47

Member
Joined
Aug 5, 2023
Posts
15
Reaction score
4
Habari ya mdaa huu viongozi mnaendeleaje, mrejesho.

Ashukuriwe Mungu wa mbinguni pia mbarikiwe Wana jf wote Kwa mawazo ushauli n.k nilikuwa kwenye wakati mgumu sana lakini hatimaye solutions imepatikana Kwa kuanza na service ambazo zimebaki na mda si mrefu kuanza na kazi katika eneo Hilo
 
Habari ya mdaa huu viongozi mnaendeleaje, naombeni ushauri.

Nina changamoto nilitaka eneo la biashara baada ya kufatilia nilipata namba ya Mmiliki baada ya hapo tukawasiliana akanambia nichague chumba akanipa gharama za chumba Kwa mwezi Tsh. 80.000/-.

Kwakua hakuwa na fedha ya kumalizia alinambia nitoe Kodi ya mwaka ambayo Tsh. 960.000 nilimtumia kwenye simu na muamala bado ninao nililipa japo hatukuonana Kwa macho ila ni mtu ninae mfahamu.

Nimemtumia pesa 5.06.2023 mpaka hii Leo tarehe 5.08.2023 fremu hajamaliza ukarabati, baada ya kuona kuwa Mimi muda unaenda sifanyi chochote na yeye hana mwelekeo wa kumaliza nilimwomba pesa Ili niangalie eneo lingine la biashara ananijibu kwamba nitafute mtu wa kumpangisha Ili nipate Kodi wakati haiwezekai na eneo mimi sio mmiliki.

Naombeni mawazo nifanye nini Ili niweze kupata pesa na kuangalia eneo lingine ndo hayo, naomba kuwasilisha.
Muongezee pesa ya mwaka mgine au nusu uliakamilishe kwa kusimamia mwenyewe.
 
Kwani milikubaliana ukishamtumia hizo pesa kwa makadirio angekua amekamilisha ujenzi ndani ya mda gani?

Kama amevuka muda basi kwa lugha nyepesi kabisa AMEKUTAPELI
 
Kwani milikubaliana ukishamtupia hizo pesa kwa makadirio angekua amekamilisha ujenzi ndani ya mda gani?

Kama amevuka muda basi kwa lugha nyepesi kabisa AMEKUTAPELI
Ilitakiwa mpaka wa mwezi 7 niwe nimeanza kupatumia
 
Hapana ila namfahamu pia muamala Bado ninao
umefanya makosa Sana, siku nyingine usimpe mtu hela kienyeji namna hiyo watu sio waaminifu tena. Hakikisha mnakuwa na mkataba wa maandish na shahidi awepo.
Kama hana hela na eneo unaona ni potential andikishaneni kisha ukarabat kwa hela yako mtakatana mwaka unaofuta. usisahau mashahid na serikali za mtaa huyo jamaa sio mwaminifu.
 
Asante sana ndugu yangu nimekuelewa vyema
 
Habari ya mdaa huu viongozi mnaendeleaje, naombeni ushauri.

Nina changamoto nilitaka eneo la biashara baada ya kufatilia nilipata namba ya Mmiliki baada ya hapo tukawasiliana akanambia nichague chumba akanipa gharama za chumba Kwa mwezi Tsh. 80.000/-.

Kwakua hakuwa na fedha ya kumalizia alinambia nitoe Kodi ya mwaka ambayo Tsh. 960.000 nilimtumia kwenye simu na muamala bado ninao nililipa japo hatukuonana Kwa macho ila ni mtu ninae mfahamu.

Nimemtumia pesa 5.06.2023 mpaka hii Leo tarehe 5.08.2023 fremu hajamaliza ukarabati, baada ya kuona kuwa Mimi muda unaenda sifanyi chochote na yeye hana mwelekeo wa kumaliza nilimwomba pesa Ili niangalie eneo lingine la biashara ananijibu kwamba nitafute mtu wa kumpangisha Ili nipate Kodi wakati haiwezekai na eneo mimi sio mmiliki.

Naombeni mawazo nifanye nini Ili niweze kupata pesa na kuangalia eneo lingine ndo hayo, naomba kuwasilisha.
hizo pesa zingine atakuwa ametumia kusolve issue zake zingine, hapo umeingia kwenye mtego hata yeye hana wasiwasi itabidi uvumilie tu. Kwanini usingekuwa karibu wakati wa umaliziaji huo. Mkubaliane kazi iliyobaki uisimamie lakini kwa ukaribu wake akijua kila kitu, ila muandikishane, kujenga nyumba ya mtu ndugu ni hatari.
 
Shukrani sana
 
Back
Top Bottom