Msaada na ufafanuzi wa sheria - PPF act 2001

Msaada na ufafanuzi wa sheria - PPF act 2001

Ti Go

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
985
Reaction score
1,004
Waana jamii forum naomba ufafanuzi wa sheria za mafao ya wafanyakazi wa yaliyokuwa mashirika ya umma - ppf act.
Kabla ya mwaka 2001 sheria ya PPF ilikuwa, kama mwanachama wa PPF atakuwa amechangia miaka 10 na kuendelea, endapo ataacha kazi basi anakuwa pensionable - atalipwa pension ya kila mwezi hadi kufa. Ilipofika mwaka 2001 serikali ikatunga sheria mpya ya kufuta kipengere hicho na kudai kuwa mtu atapaswa kulipwa pension atakapostaafu akiwa na umri wa miaka 55 na kuendelea/au akistaafu basi asubiri mpaka atimize miaka 55.
Hiyo kwangu haikuwa shida, tatizo ni sheria inapotungwa huwa hairudi nyuma - haipaswi kuwabana waliopita bali inashughulika na matendo yanayotendwa baada ya kutungwa sheria hiyo ( kumbuka retrospective na kinyume chake). Baada ya kutungwa sheria hiyo, ppf wakaitumia kuwanyima wastaafu waliostaafu kabla ya kutungwa sheria hiyo badala ya kuwabana watakaostaafu baada ya sheria kutungwa.
Najua watu wengi wanasoma jamii forum, naomba ufafanuzi wa tatizo hilo hapo juu. Ni halali kutunga sheria leo na ikatumika kuhumu matendo yaliyofanywa kabla ya kutungwa sheria, na kama ni hivyo inarudi nyuma mpaka lini ) inaenda nyuma umbali gali). Please assist, hii iliumiza watu wengi
 
Back
Top Bottom