Msaada: Nafikiria kuanzisha biashara ya duka la kuuza vifungashio na mifuko mbadala

Msaada: Nafikiria kuanzisha biashara ya duka la kuuza vifungashio na mifuko mbadala

Mr.genius

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
1,374
Reaction score
1,201
Salama wakuu? kwema? niende kwenye mada moja kwa moja.
Nafikiria kuanzisha duka la kuuza vifungashio vya bidhaa mbali mbali mfano: asali, karanga, ubuyu wengine wanawekea pilipili kiujumla wale wanaofanya biashara ya ku process na ku - pack vyakula vilivyoongezewa thamani hua wanatumia sana pamoja na mifuko ile mifuko tuliyozoea kuiita mifuko mbadala. Biashara yangu iko kwenye stage ya wazo bado, (location Morogoro mjini) hivyo nahitajji msaada wa taarifa zaidi like wapi ntapata hizo bidhaa (kama wanauza kwa jumla), mtaji kiasi gani nijiandae nao na namna biashara hiyo ilivyo kiujumla. Naamini jf ni jungu kuu halikosi ukoko waungwana mtanisaidia katika hilo.
Natanguliza shukrani.
 
Kwanini usiagize China?,unaweza nunua kifungashio mfano vike vikopo vya ubuyu kwa Bei rahisi mfano tsh 6,wewe ukaja uza tsh 200,faida kede kede
China unaagiza ila kodi yake ni kubwa maana kodi huesabiwa kwa uzito, na TRA huesabu kodi kwa 1kg= USD 2
 
China unaagiza ila kodi yake ni kubwa maana kodi huesabiwa kwa uzito, na TRA huesabu kodi kwa 1kg= USD 2

Even if still ni rahisi vifuko Mpaka vifike kg 1 ni vingi sana
 
Mkuu hakuna wanaouza kwa bei ya Jumla hapa nyumbani?
Kwanini usiagize China?,unaweza nunua kifungashio mfano vike vikopo vya ubuyu kwa Bei rahisi mfano tsh 6,wewe ukaja uza tsh 200,faida kede kede
 
Back
Top Bottom