Msaada nahitaji dawa ya stress

Hakuna..
Kunywa maji, oga na ujaribu kupumzika ukiweza kupata usingizi basi lala.
 
Ninadhani dawa kubwa ni kufahamu kitu kinachokusabishia stress kwanza, ukisha dili nacho utupe mrejesho.
 
Watafute watu wako wa karibu unaoamini wanakupenda wanakuthamini wanakujali, share nao kilichokusababishia stress...watakushauri

Na unaweza kuopt kuwa karibu nao zaidi kipindi cha stress utapata ahueni

Njia hii imenisaidia binafsi mara nyingi
 
Hakuna kitu kama hicho!!!
Kuna dawa za matokeo ya unmanaged stress...
Kama haujaathirika, solution ni kupata usingizi mzuri (atleast saa tano), ule vizuri na ufayev mazoezi angalau dakika 30 kwa siku.
 
Dawa ya stress ambayo ni temporary ni kufanya mazoezi kwa dk 30. Kama huna mudi ya zoezi chukua nanasi kipande, papai, limao, na chungwa brend pata smoothie na kunywa usiweke maji ila kidogo ya kusaidia kuzungusha brenda,.. Itakusaidia. Dawa ya stress ya permanent ni kufaham kuwa kila kitu ulicho kuwa nacho na usicho kuwa nacho ni mali ya mungu akitaka anakupa akitaka anachukua.. Iwe mali iwe watoto.. Na pia kujua kuwa kila kitu kina expire date yake iwe furaha iwe huzuni... Muhimu ni kuwa na subira na kukipa kitu muda.... Ukifaham hilo utakuwa mtu wa furaha milele kama mimi... Mfano mpenzi wako akikuacha utahuzunika kwa muda ila utajua hiyo ndo expire date yake na utasonga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…