Msaada: Nahitaji kuchukua mafao NSSF kwa haraka

Msaada: Nahitaji kuchukua mafao NSSF kwa haraka

MamaMtoi

Member
Joined
May 26, 2015
Posts
25
Reaction score
7
Wapendwa nataka kuchukua mafao yangu NSSF ila nasikia wanaweza kukuzungusha hata mwaka mzima.

Je, nitumie njia gani nifanikishe kwa haraka?
 
Utaratibu wao upo hivi
1.Nenda na barua ya resignation/termination ya employment, kwenye kanda uliyokua ukifanyia kazi, itoe kopi hio barua utawaachia wanadai wanaverify kama kweli umeacha kazi au kazi imesitishwa hii wanasema itachukua siku 2-3 kwaio kua mvumilivu
2.Baada ya hizo siku 2-3 nenda na kitambulisho chako, pia kitoe kopi hicho kitambulisho chako, pia nenda,picha za passport size 3 na form ulizo jaziwa na HR wako zinaonesha kweli umeacha kazi, michango yako na namba za risiti ya michango yako...utapewa form uijaze ndo hizo picha zinabandikwa halafu utapewa tarehe ya ahadi ya siku ya kuchukua mpunga wako mara nyingi ni wiki 3 kwenye utaratibu wa urgency nafahamu ni kwenye kwenda kusoma ili uwahi kulipa ada sana unaweza ambatanisha na admission form ya either chuo ulichochaguliwa etc inaweza chukua hata siku tatu ukapata
4. kwa kifupi huo mchakato ni wa around mwezi hivi assuming haujakutana na vikwazo vya mtandao upo down njoo kesho, au form yako bado haijasainiwa etc etc
 
Wapendwa nataka kuchukua mafao yangu NSSF ila nasikia wanaweza kukuzungusha hata mwaka mzima.

Je, nitumie njia gani nifanikishe kwa haraka?

Hakuna pesa za kukulipa saa hzi pesa zote tumechukua kwa ajili ya kampeni
Vuta subira mpaka tumalize mambo yetu

Pesa zako anza kufuatilia mwakani sikunkama leo
 
Acha kunikatisha tamaa # kzba hali umekuwa tete
 
Acha kunikatisha tamaa # kzba hali umekuwa tete

Kwamba hakuna hela hiyo ni kweli. Mwezi uliopita na huu mwanzoni watu wamepigwa sana kalenda. Cheki zilikua tayari ila account yao inasoma empty (au overdraft). Hata waliokua wakidai japo laki 2 nao kalenda ziliwahusu pia.

Ila kwamba zimekuja kwenye uchaguzi hapo sina uhakika. Nachojua serikali mwaka huu imekopa sana kwenye haya mashirika baada ya kunyimwa hela na wafadhili kutokana na sakata la ESCROW. Pia gharama za ujenzi wa daraja la kigamboni zimekula hela za kutosha tu
 
Back
Top Bottom