Madam vivian original
Nikupongeze kwa kujichanga, ili Mimi na wadau wengine hapa tuweze kukupa mwanga mzuri kabisa wa haswa gari ipi ambayo itakufaa, ukizingatia kwamba umesema ndio mara yako ya kwanza . (Bila kujali una experience au la)
Ninaweza kukushauri juu ya Dualis sawa, kwa sababu ni gari nzuri kweli kwa wanawake haswa wa kileo, ulaji mzuri wa mafuta.
Lakini,
Tunaweza sema chukua Dualis, kumbe unakaa sehemu za ndani ndani huko ambazo njia ni mbovu , sehemu ni ya milima, kipindi cha mvua utelezi
Sehemu gari inapokua inakwenda (go and return) daily ni mbali , idadi ya watu ni kubwa.
Trust Me, utakuja hapa kutulaumu wadau kwamba tumekushauri uchukue gari ambayo sio nzuri kwako.
Kumbe ni maelezo yako hayakuwa yamejitosheleza.
Tungependa utuelezee vizuri machache yafuatayo ili wadau waje kukupa muongozo sahihi zaidi.
1. Gari itakapokua inatumika zaidi
2. Umbali wa matumizi ya kila siku
3. Watu wanaopakiwa kila siku (Idadi)
4. Hali ya barabara ya itakapokua inatakiwa kupita kila siku.
Hayo ni machache ya msingi kati ya mengi, ambayo naamini ukiweza kufafanua vyema basi itakuanrahisi kupata ushauri mzuri wa gari bora kabisa itakayo kufaa.
Nawasilisha.