Msaada nahitaji kupata usajili wa biashara yangu

Sweet mangi

Member
Joined
Aug 10, 2016
Posts
14
Reaction score
5
Habari za jioni Wana JF ,Mimi ni kijana mjasiriamali ,nina jishughulisha na biashara ya kutengeneza na kuuza Milk products kama Yogurt na Cultured milk(mtindi) ila changamoto ninayopata ni baadhi ya wateja kutoamini ubora na usalama wa bidhaa hizi ,hii imesababisha niache kutengeneza kwa muda.

Nimekuja kwenu ninahitaji mnisaidie na kunishauri namna ya kupata Vibali na Leseni ya biashara kama hii.

Na pia namna ya kupata Packages bora na nzuri zilizo na nembo ya Tbs,lakini pia namna ya kupata labels na seals za kuweka kwenye hizo packages ili kuondoa mashaka juu ya ubora na usalama wa bidhaa hizo na inisaidie kutangaza zaidi bidhaa hizi

Ahsanteni sana.
 
Uwe unejiandaa kimtaji, kupeleka sample tu TBS inacost hela ya maana tu, bosi wangu mmoja anafanya biashara hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…