Msaada namna kumchukua mtoto kisheria naona mama yake ameshindwa kumlea

Msaada namna kumchukua mtoto kisheria naona mama yake ameshindwa kumlea

igihumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2017
Posts
529
Reaction score
483
Habari wanajamvi?

Nahitaji mwongozo kisheria namna ya kumchukua mtoto kwa mama yake naona ameshindwa kumlea.

Mtoto bado mdogo mama yake alidai anaweza kumlea ila nilichokiona ni tofauti sana. Mtoto bado mdogo sana ana mwaka na miezi 8 ila nilishangaa kuona mama wa mtoto anafanya kazi na mtoto anaachiwa ndugu zake. Je, hii ni sawa?

Pia hata wakati tunaishi pamoja mtoto alipendeza sana ila tangia analelewa na mama tu amedhoofika sana mtoto.

Je, sheria inanipa mwongozo gani ili niweze kumchukua mwanangu kwani mazingira anayoishi kwa sasa ni hatari kwake.
 
Tembelea ofisi ya mwanasheria/wakili iliyo karibu nawe atleast ulipe consultation fees.
 
Mtumie hela ya matumizi ili akae nyumbani alee mtoto. Unalalamika mama kufanya kazi wakati hutumi pesa ya matumizi,

Wewe ni mzazi usie wajibika, ukimchukua wewe ndio utakuwa unakaa naye 24/7 hutamwacha kwa watu wengine na kwenda kufanya kazi zako?
nilikuwa nafanya kama unavyo sema hilo la kutoa matumizi tena nilikuwa natuma pesa ya wiki nzima kila wiki kwa siku10000 ikipungua sana ni 7000 ila mwisho wasiku akaniambia kukaa nyumban kumemshinda iko hivyo mkuu.
 
Ongeza kidogo hiyo pesa atakaa nyumbani na mtoto atapendeza
Nilikuwa nafanya kama unavyosema hilo la kutoa matumizi tena nilikuwa natuma pesa ya wiki nzima kila wiki kwa siku 10000 ikipungua sana ni 7000 ila mwisho wa siku akaniambia kukaa nyumbani kumemshinda iko hivyo mkuu.
 
Aisee kwahiyo ikitokea umepata matatizo umeugua au umepata tatizo lolote kama ajali unategemea atafanyaje? Mbona wamama wengine wanaacha watoto wao na house gal kuanzia wakiwa na miezi mitatu na kuendelea kwenda kazini. Mimi sioni shida hata kama unamtumia mama hela sio ya kumtunza yeye ni ya kumtunza mtoto.

ashangaa unalalamika mtu akijitafutia hela yake ulitaka atoe hela hiyo hiyo kutuma kwa ndugu/jamaa/marafiki? Anapaswa ajitafutie na chake na kukaa tu unamtegemea mtu si sawa. Inavyoelekea unampenda na unamuonea wivu mtoto wa miezi 8 bado ananyonya mwache hata kama anaachwa lakini analelewa na mamaake ingekuwa anakusumbua hpo ndio lakini amekuambia hawezi kaa nyumbani uyo ni mpambanaji acha kufuatilia maisha yake wakati umeshatengana nae.
 
Kwa hiyo.kama unatuma 10,000 mama mtoro akae ndani kisa unatuma 10,000- 7,000?????

Halafu hiyo ni kwa mtoto na sio mama mtoto

Wewe unayetaka kumchukua huyo mtoto utakaa nae nyumbani umlee au utaachia ndugu/housegirl amtunze wakati upo kwenye kutafuta??????
 
Back
Top Bottom