Msaada: Namna kupata leseni ya biashara

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Wana JF,

Naomba mwenye uzoefu na kitu hicho anipe utaratibu.Nimeamua nataka kuwa mfanyabiashara.
 
Nenda TRA watakupa TIN namba baada ya hapo watakufanyia makadirio ya biashara yako. Baada ya hapo utaenda manispaa nao watakufanyia makadirio.
 
Kwa hiyo 1 sijui unamaanisha nini!Ila kila niliyemuuliza alinijibu malipo ni mara 2,yaani ya leseni kule halmashauri pamoja na tin number kule TRA.
 
Utaratibu ni rahisi,
Unaenda TRA iliyo Karibu nawe unapatiwa TIN bure,Na kufanyiwa makadirio kwa ajili ya malipo ya Utakaso wa Kodi,au taxi clearance certificate ambayo utalipia.
Baada ya kupata T.C yako,utaenda nayo katika ofisi yoyote ya halmashauri iliyo ktk eneo lako la biashara Na kujaza fomu ya maombi ya biashara husika Na Afisa biashara atakufanyia makadirio kwa ajili ya Leseni yako kutokana Na maombi yako.
Hatua hii inahusisha uwepo wa nyaraka MF. Tin,t.c Na kama ni kampuni iliyosajiliwa unaweka Na mou+ incorporation certificate au vyeti vya usajiri toka brela.
Unaenda kulipia benk Na kurejesha slip kwa ajili ya mfumo wa malipo ya kielektrinika Na unaandaliwa Leseni yako.
 
Nyengeza:-
1.Malipo yanayofanyika Tra ni kwa mapato ya serikali Kuu
2.Malipo yanayolipiwa halmashauri zote nchini ni kwa ajili ya halmashauri zenyewe ktk majukumu mbalimbali ya kijamii ie ujenzi wa Barbara,madarasa,hospitality nk
 
Nyengeza:-
1.Malipo yanayofanyika Tra ni kwa mapato ya serikali Kuu
2.Malipo yanayolipiwa halmashauri zote nchini ni kwa ajili ya halmashauri zenyewe ktk majukumu mbalimbali ya kijamii ie ujenzi wa Barbara,madarasa,hospitality nk

Mfano tayari TIN namba ninayo, kuna haja ya kurudi tena TRA!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…