Msaada namna ya ku-renew Leseni ya biashara kupitia Tausi Portal

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
474
Reaction score
622
Habari za leo wakuu,

Mimi ni kijana wenu mhangaikaji. Leseni yangu ya biashara ya hardware imefikia ukomo, na nilihitaji kuirudia kupitia Tausi Portal. Changamoto niliyonayo ni kuwa sioni sehemu ya kufanya urudishaji wa leseni hiyo.

Nimefuata hatua zote hadi ninapofika sehemu yenye vipengele viwili:

1. Principal Business Licence
2. Subsidiary Business Licence

Hapo ndipo napokwama, wakuu. Mwenye ujuzi wa namna ya kuendelea kutoka hapo, naomba anisaidie kwa maelekezo.

NB: Akaunti ya TAUSI PORTAL ninayo na ipo active.

natumaini nitasaidika katika hilo. natanguliza shukrani
 
Hii ni lazma iwe imeshaexpire yaani suki moja mbele baada ya leseni kuisha mda wake ndio unaweza kurenew. Utaenda hapo kwenye 'my licenses' kisha utaona option ya 'renew' ambapo unaambatana mkataba wa pango, tax clearance pamoja na ID yako.

Kila la kheri
 
Shukrani sana mkuu ngoja nifuatishe hatua hizi naamini nitafanikisha
 
Huwezi fanya tax clearance mtandaoni?
 
Huwezi fanya tax clearance mtandaoni?
Tax clearance inatolewa na TRA kumaanisha hudaiwi kodi kwenye hiyo biashara yako, "clearance".

Pale wanakupa cheti, anayekitoa ni TRA. Shughuli za kukifanya kitoke zinawezwa fanywa na mtu binafsi au mtaalamu wa kodi ila anayethibitisha kuwa uko cleared ni TRA. Na anatoa huo uthibitisho kwa kutumia hiyo Tax Clearance Certificate.

Hivyo, huwezi pata certificate online maana huwezi jifanyia assessment mwenyewe kwamba sidaiwi na TRA. Fika ofisi za TRA karibu yako.
 
Tax certificate zilitakiwe ziwe na namba ya utambulisho unique ambayo utakopokuwa una log nayo ikupe specification juu ya status za mfanyabiasha na madeni yake aidha hadaiwi,still we have a journey
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…