Msaada namna ya kubadili umiliki wa gari

Msaada namna ya kubadili umiliki wa gari

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
1,595
Reaction score
3,416
Wakuu naomba msaada wa kujua kubadili kadi ya umili wa gari
1. Gari ina cc 1990 ya mwaka 2000
2. Nimenunua kwa mtu wa Mwanza mwaka jana,ila mimi naishi chanika dar
3. Niende TRA ipi kwa hapa Dar?
4. Nilinunua 8500,000/=niandae kama sh ngapi?
5. Nina karatasi ya mauziano ya kawaida tu ya mkono,na picha za muuzaji,na namba zake za simu.msaada wakuu.
 
Wakuu naomba msaada wa kujua kubadili kadi ya umili wa gari
1.Gari ina cc 1990 ya mwaka 2000
2.Nimenunua kwa mtu wa Mwanza mwaka jana,ila mimi naishi chanika dar
3.Niende TRA ipi kwa hapa Dar?
4.Nilinunua 8500,000/=niandae kama sh ngapi?
5.Nina karatasi ya mauziano ya kawaida tu ya mkono,na picha za muuzaji,na namba zake za simu.msaada wakuu.
Tra yyt andaa kitu km 300k
 
Attachments

  • 20210712_140607.jpg
    20210712_140607.jpg
    253.7 KB · Views: 179
Utaratibu mpya wa TRA
1.Kuwepo mkataba wa mauziano ulioandaliwa na mwanasheria.Achana na vile vimkataba mshenzi tunavyosainishana.
2.Kiapo cha kukiri umiliki wa gari kutoka kwa muuzaji.Kiandaliwe na mwanasheria
3.Picha P size na kitambulisho leseni au NIDA ya muuzaji na mnunuaji.
4.Hati ya ukaguzi wa gari kutoka kwa vehicle inspector.Hapo lazima akague gari kwanza.
5.Kadi ya gari yenye jina la muuzaji.
 
Aliyekuuzia alitakiwa afanya mchakato wa kubadilisha umiki, ni mzembe sana. Angekutana na wahuni wanatumia hiyo gari kwenye mambo mabaya alafu anakuja kukamatwa yeye.

Hiyo gari ingekuwa ni yangu nisingeangaika kubadilisha umiliki.
 
Siku hizi umiliki si anabadilisha muuzaji?
Nikuuzie halafu nikuhangaikie kukubadilishia umiliki? Ya wapi hiyo? Wewe uliyechukua zigo kazi kwako kuprove lako nisije kukugeuka.

Na mimi niliyekuuzia kazi yangu ni kuprove sio langu tena; ukienda kuua huko lako hilo.

The best I can do ni kumlipa wakili aandike hati ya kuhamisha umiliki from me to you that's all hayo mengine yako mnunuzi. Na hati ni mali yangu sio yako.

Ni sawa na ununue kitu halafu risiti umuachie muuzaji! Watanzania tuna akili za kindezi sana.
 
Aliyekuuzia alitakiwa afanya mchakato wa kubadilisha umiki, ni mzembe sana. Angekutana na wahuni wanatumia hiyo gari kwenye mambo mabaya alafu anakuja kukamatwa yeye.

Hiyo gari ingekuwa ni yangu nisingeangaika kubadilisha umiliki.
Uliyenunua it's your burden kuprove ni yako! Ununue mali halafu risiti umuachie muuzaji? Akili matope?
 
KWA GHARAMA TU

1. Swali: Chombo cha moto ni nini?
Jibu : Ni chombo kinachotumika katika usafirishaji ardhini, ambavyo ni pamoja na Magari, pikipiki na bajaji.

2. Swali: Nikitaka kununua gari kwa mtu taratibu zipoje?
Jibu : Unapaswa ufike ofisi ya TRA na picha ya pasipoti ya muuzaji, ripoti ya ukaguzi kutoka kwa trafiki, barua ya muuzaji kuhusu mabadiliko ya umiliki wa gari, picha yako ya pasipoti, kadi halisi ya gari, hati ya kiapo ya muuzaji, gari kufika TRA kwa ajili ya ukaguzi, mkataba wa mauziano uliothibitishwa na mwanasheria na upewe risiti ya EFD kutokana na huduma ya kisheria.

3. Swali: kumwakilisha mtu kwenye taarifa za uhamishaji wa chombo unaruhusiwa?
Jibu : Ndiyo kwa kampuni au taasisi unaruhusiwa kwa mwakilishi kuleta idhini maalum ya kisheria (Power of Artoney) ya kuthibitisha uwakilishi wake lakini kwa mtu binafsi anapaswa awepo mhusika mwenyewe.

4. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa gari ni shilingi ngapi?
Jibu : Ada ni shilingi 50,000 + ada ya nakala ya kadi ni shilingi 50,000 +ushuru wa stempu ambayo ni 1% ya bei ya gari.

5. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa bajaji, Je?
Jibu : Ada ni shilingi 27,000 + ada ya nakala ya kadi shilingi 30,000 , ambapo jumla ni shilingi 57,000.

6. Swali: Gharama ya kuhamisha umiliki wa pikipiki nao upoje?
Jibu : Ada ya uhamisho ni shilingi 27,000 + ada ya nakala ya kadi shilingi 20,000, ambapo jumla ni shilingi 47,000.

7. Swali: Kuna ulazima wa kubadilisha taarifa za umiliki TRA?
Jibu : Ndiyo, unapaswa kubadili taarifa za chombo TRA ili umiliki uhame kutoka kwako kwenda kwa mtu mwingine la sivyo kuna athari zinaweza kutokea.

8. Swali: Athari za kutobadili umiliki au taarifa ya chombo cha moto ni zipi?
Jibu : Athari zinazoweza kutokea ni
(i) Mmiliki wa awali anaweza kuwajibishwa endapo chombo kitatumika kwenye uhalifu.
(ii) Mmiliki mpya atakosa malipo ya fidia kutoka bima.
(iii) Mmiliki mpya atakosa uhalali wa kutumia chombo hicho kama dhamana ya kukopa.
(iv) Mmiliki awali atawajibika endapo mmiliki mpya atakopa kwa kutumia chombo hicho.
 
Duh asee. Sasa mfano mimi ni mmiliki wa tatu. Afu yule mmiliki wa pili hakubadilisha umiliki akaniuzia hivyo hivyo. Nami nikatumia baada ya muda nataka nibadili kumfata aloniuzia akaniambia aliyemuuzia hayuko ndani ya nchi.
Na hana mawasiliano naye kwa sasa.
Je naweza tumia mkataba wa mauziano na mmiliki wa pili kubadilisha umiliki hali ya kuwa kwenye kadi kunasoma jina jingine?
 
Utaratibu mpya wa TRA
1.Kuwepo mkataba wa mauziano ulioandaliwa na mwanasheria.Achana na vile vimkataba mshenzi tunavyosainishana.
2.Kiapo cha kukiri umiliki wa gari kutoka kwa muuzaji.Kiandaliwe na mwanasheria
3.Picha P size na kitambulisho leseni au NIDA ya muuzaji na mnunuaji.
4.Hati ya ukaguzi wa gari kutoka kwa vehicle inspector.Hapo lazima akague gari kwanza.
5.Kadi ya gari yenye jina la muuzaji.
Je kadi ya gari ikiwa ni copy iliyokuwa certified?
Wataweza kubadili?
 
uzi
Utaratibu mpya wa TRA
1.Kuwepo mkataba wa mauziano ulioandaliwa na mwanasheria.Achana na vile vimkataba mshenzi tunavyosainishana.
2.Kiapo cha kukiri umiliki wa gari kutoka kwa muuzaji.Kiandaliwe na mwanasheria
3.Picha P size na kitambulisho leseni au NIDA ya muuzaji na mnunuaji.
4.Hati ya ukaguzi wa gari kutoka kwa vehicle inspector.Hapo lazima akague gari kwanza.
5.Kadi ya gari yenye jina la muuzaji.
uzi wa zamani.. hawa wapigaji hawana cha utaratibu mpya wala nini..kama hutaki process mwendo ni ulele andaa bahasha unarudi na kadi mpya siku hiyo hiyo
 
uzi

uzi wa zamani.. hawa wapigaji hawana cha utaratibu mpya wala nini..kama hutaki process mwendo ni ulele andaa bahasha unarudi na kadi mpya siku hiyo hiyo
Fafanua mkuu
 
Back
Top Bottom