Msaada: Namna ya kumshauri aliyeathirika kisaikolojia kwa ku-abort

Msaada: Namna ya kumshauri aliyeathirika kisaikolojia kwa ku-abort

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Nasalimia kwa adabu zote stahiki. Bahati mbaya kiswahili chetu hakijawa na salama "universal" na mjadala wa "shikamoo" hatujawai kuufunga!

Ila bado napigia chapuo...salaam aleikhum!

Humu JF ni familia. Tunawekana sawa kila mtu na karama yake, elimu, maarifa na ujuzi!

Hoja yangu ni huyu binti ambae bila kujari past yake (maana kila mtu ana shits zake za nyuma na binafs si mzuri wa kuhukum) anasumbuliwa na kitendo cha kutoa mimba.

Tatizo ni kwamba suala limemuathiri sana kisaikolojia kwa kujiona mkosaji dhidi yake na Mungu. Hana kifua cha kujipoza kwa lililokwisha kuwa!

Je, ni maneno/mbinu gan naweza kumshauri aweze kufuta kumbukumbu asonge mbele?

Mana ni kama anahisi hatia ni kubwa na inamtafuna sana kisaikolojia.

Nahitaji msaada wa kuanzia alipo sio ilikuwaje!

Naamin tu mi sijui lakin kuna wanaojua mana hii ni taaluma pia. Naheshim taaluma kama ninavyoheshim uzoefu!
 
Anyway, ulitakiwa kunilipa ila nahitaji kutenda jambo jema in turn nikatoboe interview so hii ni barter trade hapa.

Ukiwa unatoa ushauri usimuonyeshe njia. Muache njia aione mwenyewe.

Kua msikilizaji zaidi.

Kutana naye sehemu ambayo mpo comfortable, mnaonana na kama unaweza fanya mazungumzo yawe ni marafiki mnaongea.

Swali lako laweza kua. Sasa nitamfanyaje aione njia mwenyewe?

Hapa tumia Reverse Psychology. Acha yeye ndiye awe anaongea juu ya ishu yake, acha yeye pia aseme ni muda gani alihisi suluhisho ni abortion na kwanini.

Acha afikie sehemu aseme kua naona ni dhambi kwaajili ya ishu moja au mbili au tatu. Ukichanga karata vizuri yeye mwenyewe anaweza akasema "Ila nahisi nikifanya . . . . nitakaa sawa"

Kua slow, usimpressure, inawezekana usipate suluhisho siku ya kwanza mtakayokaa so acha iwe endelevu.

Kama anataka kutrace tatizo kuanzia akiwa young fanya hivyo pia.

NB: Sina fancy terms kwakua nimemaliza chuo kitambo nimesahau baadhi ya ishu.

Good luck
 
Kwan
Nasalimia kwa adabu zote stahiki. Bahati mbaya kiswahili chetu hakijawa na salama "universal" na mjadala wa "shikamoo" hatujawai kuufunga!
Ila bado napigia chapuo...salaam aleikhum!
Humu jf ni familia. Tunawekana sawa kila mtu na karama yake, elimu, maarifa na ujuzi!
Hoja yangu ni huyu binti ambae bila kujari past yake( maana kila mtu ana shits zake za nyuma na binafs si mzuri wa kuhukum), anasumbuliwa na kitendo cha kutoa mimba.
Tatizo ni kwamba suala limemuathiri sana kisaikolojia kwa kujiona mkosaji dhidi yake na Mungu. Hana kifua cha kujipoza kwa lililokwisha kuwa!
Je, ni maneno/mbinu gan naweza kumshauri aweze kufuta kumbukumbu asonge mbele?
Mana ni kama anahisi hatia ni kubwa na inamtafuna sana kisaikolojia.
Nahitaji msaada wa kuanzia alipo sio ilikuwaje!
Naamin tu mi sijui lakin kuna wanaojua mana hii ni taaluma pia. Naheshim taaluma kama ninavyoheshim uzoefu!
Kwanza ametoa ngapi na ana umri gani na kaolewa na vipi anachangamoto za kutokushika mimba kwa sasa ili ujue unaanzaje kumpatia ushauri
 
Time heals,kwa sasa aendelee kujutia kitendo chake na akusudie kutokutoa mimba tena.
 
Apate mimba tena. Akiweza kubeba atahisi amesamehewa dhambi zake. Problem solved!
 
Kwan

Kwanza ametoa ngapi na ana umri gani na kaolewa na vipi anachangamoto za kutokushika mimba kwa sasa ili ujue unaanzaje kumpatia ushauri
Alitoa akiwa chuo. Hajaolewa. Hana tatzo la uzaz.
Sema amejikita sana dini na bado kashindwa kustahimili kosa lake. Ni kama hana raha muda wote juu ya kitu kile kile!
 
Alitoa akiwa chuo. Hajaolewa. Hana tatzo la uzaz.
Sema amejikita sana dini na bado kashindwa kustahimili kosa lake. Ni kama hana raha muda wote juu ya kitu kile kile!
Wewe bado kula kulala kwa wazazi?
 
Alitoa akiwa chuo. Hajaolewa. Hana tatzo la uzaz.
Sema amejikita sana dini na bado kashindwa kustahimili kosa lake. Ni kama hana raha muda wote juu ya kitu kile kile!
Atubu kwa Mungu wake. Aache dhambj atende ya kumpendeza Mungu. Aende kwa mchungaji wa kanisa analosali amuambie anataka kutubu ana mzigo moyoni unaomtesa nadhani matokeo mazuri yatakuja.
 
Back
Top Bottom