Msaada namna ya kumuandaa bata

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
787
Reaction score
526
Salaams.

Nahitaji kuchinga bata wangu walau leo nami nijinafasi lakin sijui namna gani ya kumuandaa ili asiwe na shombo.

Msaada pls.
 
Bata analiwa? achana na hiyo kitu....! bata ni pet kama walivyo paka na mbwa.......
 
Mchemshe pamoja na vitunguu saumu baada ya hapo mkaange hatakuwa na shombo pia ndimu nyingi sana husaidia pia..
 
Mchemshe pamoja na vitunguu saumu baada ya hapo mkaange hatakuwa na shombo pia ndimu nyingi sana husaidia pia..

Asante Ndetichia.

Na namna rahisi ya kumunyonyoa?
 
Mwenye shibe ndo anachagua msosi
 
Duh kula bata ama nguruwe inabidi uwe na deficity ya kinyaaa
 
Salaams.

Nahitaji kuchinga bata wangu walau leo nami nijinafasi lakin sijui namna gani ya kumuandaa ili asiwe na shombo.

Msaada pls.
ukitaka asiwe na shombo, mwekee chumvi, thoum, tangawiz na limao usisahau, kisha mbanike kwanza. baadae uendelee na design zako za upishi
 
akohi teleka maji jikoni hadi yachamke alafu mdumbukize pata kwa dakika 1 ukiwa umemshikilia ila manyoya yalainike alafu mtoe anza kumnyonyoa manyoya fanya hivo hadi kumaliza.....

Zingatia maji yasiwe moto sana atababuka....

Wakati ushamsafisha ndani yaani kumtoa machango ya nyongo muweke kwenye sinia....katakata malimau alafu tumia malimau hayo kumsugua taratibu kila kona inasaidia kuondoa ile harufu.....
 
Last edited by a moderator:
Nawashukuru sana nyote kwa michango yenu, nimefarijika sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…