Msaada namna ya kupika maharage matamu

Msaada namna ya kupika maharage matamu

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
1,576
Reaction score
3,094
Napenda kuwasalimu ndugu zangu wa JF.

Nimekuwa nikipika maharage lakini nashindwa kuyafanya yawe matamu ila akipika mwingine naona ni matamu.

Nashindwa pia kujua kubalance mchuzi ninapounga napenda mchuzi mwingi lakini najikuta nikipika Mimi huo mchuzi Unakuwa Mbaya.

Naombeni msaada pamoja na namna ya kuweka viungo na viungo vya kutumia kufanya mambo yawe bul bul
Nathamini mchango wowote.
 
Viungo:
  • Kitunguu
  • Karoti
  • Hoho
  • Pilipili manga (kidogo sana)
  • Kitunguu Swaum
  • Mafuta.
Jinsi ya kuandaa:
  1. Katakata viungo vyako vyote kwenye shape ndogo ndogo.
  2. Weka mafuta kwenye sufuria yako yakipata moto Anza kukaanga vitunguu.
  3. Vitunguu vikianza kubadilika rangi weka kitunguu saumu na uendelee kukoroga.
  4. Then weka karoti na pilipili manga changanya.
  5. Weka hoho zako pamoja na maharage yako. Changanya mchanganyiko wako vizuri na ufunike uache uchemke (Kama dakika 2-3) then funua weka chumvi kiasi chako na ufunike tena.
  6. Baadae ya kama dakika 1 funua na maharage yako yapo tayari.
NB: hizo process zote zinafanyika baada ya kuwa umeisha chemsha maharage yako na yakalainika vizuri.
Pia unaweza ongezea nazi kama utapenda.
Pia sijaweka vipimo maana sijui WINGI wa maharage yako
 
Napenda kuwasalimu ndugu zangu wa JF.

Nimekuwa nikipika maharage lakini nashindwa kuyafanya yawe matamu ila akipika mwingine naona ni matamu.

Nashindwa pia kujua kubalance mchuzi ninapounga napenda mchuzi mwingi lakini najikuta nikipika Mimi huo mchuzi Unakuwa Mbaya.

Naombeni msaada pamoja na namna ya kuweka viungo na viungo vya kutumia kufanya mambo yawe bul bul
Nathamini mchango wowote.
Hujaowa tuu?
 
Oa mkuu au unataka kuwa hotelia? Hayo mambo ya kupika chakula kitamu ni shughuli za wadada japo wanaume tunapika ila hatuhangaiki kupika kiwe kitamu Bali kiive kishungulikiwe, mambo mengine yaendelee.
 
Back
Top Bottom