Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nina ujauzito haujamaliza hata mwezi, tatizo langu matiti yananiuma sana, je nifanyeje ili kumaliza tatizo hili bila kuathiri ujauzito?. Nimeenda Hospitalini nikaabiwa eti yataacha yeyewe, je ni kweli?
Nina ujauzito haujamaliza hata mwezi, tatizo langu matiti yananiuma sana, je nifanyeje ili kumaliza tatizo hili bila kuathiri ujauzito?. Nimeenda Hospitalini nikaabiwa eti yataacha yeyewe, je ni kweli?
Nashukuru sanaHabari yako,
Kwanza hongera kwa kuwa u mjamzito...
Pili nadhani huna tatizo lolote na kuuma huko kwa matiti si ugonjwa bali ni jambo la kawaida kwa mwanamke mjamzito huwa na hali hiyo kwenye hatua za mwanzoni mwa ujauzito...
Hali kama hiyo huwa inafanana kwa mbali na namna matiti yanavyouma kwa mwanamke anayekaribia kupata damu ya hedhi...
Sababu kubwa ni kutokana na mabadiliko ya vichocheo vya estrogen and progesterone hivyo damu nyingi huelekea kwa maitit na kuyafanya yawe kama yamejaa"kuvimbiana", yenye kuwa na hisia ya hali ya juu haswa uguswapo na kuuma...
Tegemea kupata hali hiyo ndani ya wiki 4 hadi 6 za mwanzo wa ujauzito na taratibu itapotea na utakuwa sawa baada tu ya "trimester" ya kwanza.
Nashukuru sana
Hapo kwenye red sijakupata nakuomba unifafanulie vizuri.Amini ulichoambiwa na daktari hakika yataacha! By the way, ulimuona GP au Gynecologist?
Hapo kwenye red sijakupata nakuomba unifafanulie vizuri.
Shukurani.Sorry dada JAK, nilikuwa kwenye maandalizi ya sikukuu toka jana mchana! Nadhani utakuwa ushapata maelezo mazuri kwa wadau juu ya hali uliyoieleza. Kwa lugha nyepesi kuelewa, GP au General Practitioner ni daktari asiye na specialization, wakati gynecologist ni daktari aliye-specialize kwenye afya ya uzazi!