Msaada: naomba kufahamishwa namna ya kuongeza jina la 3 kwenye vyeti.

Msaada: naomba kufahamishwa namna ya kuongeza jina la 3 kwenye vyeti.

Differential Equations

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
204
Reaction score
200
Habari za Leo ndg zangu

Naomba kupewa process ya kuongeza jina la 3 kwenye vyeti na garama zake kwa wanaofahamu.

Thanks.
 
Nadhani jamiiforums ina wanasheria wa kutosha ila uzi huu haujapata majibu stahiki.
Wataalamu wa sheria mwageni ujuzi wenu tafadhali
 
Habari za Leo ndg zangu

Naomba kupewa process ya kuongeza jina la 3 kwenye vyeti na garama zake kwa wanaofahamu.

Thanks.

Kimsingi haiwezekani kuongeza jina kwenye cheti ambacho tayari umeshapewa (i.e. Cheti cha kuzaliwa au cha kuhitimu elimu.
Kama umekuwa ukitumia majina mawili (i.e. Differential Equations) na sasa unataka unataka kutumia majina matatu (i.e. Differential Algebra Equations), unachoweza kufanya ni kuapa kiapo ambacho utaorodhesha majina uliyokuwa ukitumia (hayo yaliopo kwenye vyeti) na utayakana hayo majina na kuelekeza watu wote wawe wanakutambua kwa majina yako mapya (matatu). Mwisho unapaswa kupeleka kiapo chako kwa msajili wa nyaraka ili kisajiliwe na uwe unatambulika kisheria kwa majina yako mapya.

Kuhusu gharama:
1. Gharama ya kuandaa kiapo (hii ni mapatano kati yako na mwanasheria atakae kuandalia)
2. Gharama ya mhuri wa kiapo (kama kimeandaliwa na wakili basi atachanganya na gharama za 1 hapo juu) (alternatively unaweza kwenda mahakamani na kugongewa muhuri, gharama ni mapatano kati yako na karani)
3. Gharama za usajili kwa msajili wa nyaraka (kwa sasa ni TZS 32,000)

Muda:
Process nzima itachukua kama siku 14 hivi mpaka kukamilika kwa usajili wa kiapo.
 
kaape kwa mwanasheria yeyote aliye karibu nawe kuna either deep poll au affidavit ya jina hapo.

Hata mm kwenye lain yangu ya simu Ina majna ambayo sio yangu na niliambiwa niende mahakaman ila hata skupewa utaratbu kamili so sjui nianzie wapi pia mkuu msaada plz
 
Back
Top Bottom