Shukurani
Kuna kingine, je hawa wadhamini huwa wanatafutwa baada ya kufuzu Usaili au hata kabla?
Mkuu
Mwifwa amejitahidi kukuelimisha hapo juu; na yuko sahihi kabisa.
Wadhamini hawa ni watu ambao ni lazima wawe wanakufahamu vizuri tabia zako na sifa zako za kitaaluma. Wanaweza kuwa walimu wako waliokufundisha chuoni lakini wawe tu wanakufahamu vizuri na wawe tayari kuelezea sifa zako wakiombwa kufanya hivyo. Kwenye kazi siriazi mwajiri anaweza hata kwenda kuongea nao uso kwa uso badala ya maongezi tu ya kwenye simu.
Katika CV yako kule mwisho kabisa ndiyo yanakaa majina ya hawa wadhamini pamoja na habari zao zote za mawasiliano (namba za simu na emails zao). Kwa kawaida huwa ni watu watatu.
Inashauriwa sana usiweke tu ndugu zako au washikaji wa kijiweni lakini wawe watu wanaokujua kitaaluma kuhusiana na kile ulichosomea.
Hawa unakwenda na unawaomba personally kuwa unataka wawe wadhamini wako. Na hakikisha wanakukumbuka hata baada ya kuondoka chuoni (kama ni maprofesa wako). Hii ina maana kuwa ni lazima uwe na mawasiliano nao ya hapa na pale. Unaweza kuwa consistent kwa mfano kila mwaka wakati wa sikukuu za Krismasi au Eid unawatumia kadi ya kuwatakia mema ukijitambulisha wewe ni nani.
Ukiomba kazi (na ukapita kwenye mchujo) inabidi uwatafute na kuwaambia kuwa mimi ni fulani, ulinifundisha kozi fulani mwaka fulani na wewe ni mdhamini wangu. Nimeomba kazi mahali fulani na pengine waajiri watakuja kwako kuuliza sifa zangu hivyo nakupa heads up.
Na kwa vile wengi wao wanaweza kuwa bize sana basi unaweza ukajiandikia mwenyewe sifa zako za muhimu ambazo unataka wamwambie mwajiri wako mtarajiwa. Na wadhamini wengine watakwambia uandike hiyo barua yenye sifa zako mwenyewe halafu uwatumie na wao wataongezea tu vitu vichache kwa sababu wewe ndiyo unajijua zaidi kuliko mtu ye yote.
Recommendation letters nzuri kutoka kwa watu muhimu kama maprofesa wako ni kitu cha muhimu sana katika maombi yako ya kazi.
Mwaka fulani niliwahi kukaa kwenye selection committee ya shirika moja lililokuwa linatoa ufadhili kwa wanafunzi kutoka Afrika na recommendation letters zilikuwa zinachangia point 30 kwenye mchujo mzima. Unachukua recommendation letter kutoka kwa muombaji wa Nigeria, Kenya au Afrika Kusini unakuta ina kurasa tatu yaani imeandikwa vizuri sana mtu unasoma unapata picha ya mwombaji. Unachukua ya mwombaji kutoka Tanzania unakutana na " The applicant was a student in my junior Microeconomics class and he did well. I hope you will consider his application. Sincerely Prof. Ngwale." Ni wazi yule mwenye recommendation letters nzuri atapewa nafasi zaidi.
Naweza kukuongoza vizuri katika issues hizi na hata kukurekebishia CV yako ili iwe ya kimataifa zaidi ukitaka kwa sababu nina uzoefu wa kina na mambo haya.
Kila la heri [emoji1545][emoji1545][emoji1545]