Msaada: Naomba kujuzwa utaratibu wa kuvunja ndoa ya kiserikali

Msaada: Naomba kujuzwa utaratibu wa kuvunja ndoa ya kiserikali

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Mimi na mke wangu tulifunga ndoa ya kiserikali about 2 years ago.

Hatujawahi kuishi pamoja ni mwendo wa mikoa tofauti.

Kuna misunderstanding za hapa na pale tunasuluhishana maisha yanasonga mbele

Hivi karibuni mke kang'ang'ania tuvunje ndoa. Nimemwambia acheck utaratibu ukoje akadai talaka anayoitaka.

Je utaratibu wa kisheria ukoje hapo kukamilisha jambo hili.??
 
Kwa kawaida na kisheria Ndoa zote zinavunjwa na Mahakama kwa nchini Tanzania. Ukisoma kifungu cha 99, Cha sheria ya Ndoa Juzuu Namba 29 /2002, Kila mwana ndoa anahaki ya kuomba kuvunja ndoa yake Mahakamani kwa kupeleka maombi Mahakamani.

Na hapa haijalishi ni ndoa iliyofungwa vipi,, ? hata ikiwa ya Bomani. Na Mahakama itavunja ndoa tu ikiwa itathibitika kwamba ndoa hiyo kweli haiwezi kurekebishwa,(the marriage has been broken irreparably).

TARATIBU ZA KUFUATWA
  1. Kwanza ni lazima mwanandoa anayetaka kuvunja ndoa awe na sababu za Msingi zinazonyesha kwamba ndoa kweli imevunjika na haiwezi kurekebishika. Mfano wa sababu za kuvunja ndoa zinaweza kuwa,,, Umalaya wa mwanandoa mwenza, ukatili hapa kipigo inaweza pia kuwa alama ya ukatili huo, kutelekezwa kwa mwanandoa.
  2. Lazima mwanandoa aanzie Baraza la usuluhishi la ndoa, kwa kupeleka malalamiko yake huko, inaweza kuwa kanisani kwako,,Baraza la kata , au Baraza la usuluhishi la ndoa lililopo pale Wizara ya Ustawi wa Jamii.
  3. Lazima Miaka miwili iwe imepita tangu kufungwa kwa ndoa kati ya wana ndoa.
  4. Akishapata karatasi ya Baraza la usuluhishi ambayo inasema wameshindwa kusuluhisha hiyo ndoa, ndipo anaweza sasa kufungua kesi Mahakamani kuomba kuvunjwa kwa ndoa. Na hapa inaweza kuwa Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu mkaazi, au Mahakama Kuu ya Tanzania.
  5. .Mambo ya muhimu wakati wa kuvunja ndoa ambayo pia Mahakama itayaangalia ,, ni matunzo na nani ataishi na watoto, Mgawanyo wa mali kwa wanandoa.

Haya ni kwa kifupi ,,kama bado hujatosheka mtafute mwanasheria aweze kukuongoza katika haya,,kwa sababu kuna kitu kinaitwa in every general Rule there is Exception.

Credit: mwimbule
 
ndoa za kuishi mbali mbali zinaitwa NDOA HEWA.

Hizo ndoa huwa hazidumu.

Ukienda pale mahakama ya ndoa na mirathi temeke kesi nyingi za talaka ni za wanandoa wanaoishi mikoa mbali mbali.

Unakuta mume dodoma mke yupo dar ama mume mbeya mke yupo kahama. Hizo ndoa zinavunjika sana.

Wafanyakazi wa mahakama pale wanazipachika jina la Ndoa hewa
 
ndoa za kuishi mbali mbali zinaitwa NDOA HEWA.

Hizo ndoa huwa hazidumu...
[emoji2][emoji2][emoji2]kweli hizi ndoa hewa maana mi sijawahi kufaidia ladha ya ndoa na kukaa na mke zaidi ya migogoro miaka nenda rudi
 
Mimi na mke wangu tulifunga ndoa ya kiserikali about 2 years ago.

Hatujawahi kuishi pamoja ni mwendo wa mikoa tofauti

Kuna misunderstanding za hapa na pale tunasuluhishana maisha yanasonga mbele

Hivi karibuni mke kang'ang'ania tuvunje ndoa. Nimemwambia acheck utaratibu ukoje akadai talaka anayoitaka.

Je utaratibu wa kisheria ukoje hapo kukamilisha jambo hili.??
Aende mahakamani akaombe umpe talaka
 
mwambie asikupotezee muda wako
Na kukuletea usumbufu usokua wa lazma

Anataka talaka,yeye ndo afate taratibu
Utakuja kusaini tu kuhitimisha takwa lake.
Na ndo nlikua nafikiria hii kitu maana yeye ndo king'ang'anizi wa talaka
 
Sijui Ni Mimi TU au vipi?

Kiukweli Sijawahi kua muumini wa long distance relationship,hasa ndoa[emoji848]
Lengo la kuoa ni lipi, ikiwa mwenzi wako hauishi nae?

Long distance marriage/ relationship, hazina tofauti na ubachela tu 😅
 
Back
Top Bottom