Ili ufanikiwe kwenye kilimo kunahitaji vitu 3
1.Usimamizi.
Unao muda wa kutosha wa kuweza kusimamia shughuli zako? Ukikosa muda bora usilime kwa sababu utaibiwa.Wafanyakazi/Vibarua wanaiba sana kuanzia mbegu,mbolea,madawa na mazao yenyewe.
2.Uzoefu.
Hilo zao unalotaka kulima unalifahamu,unajua utunzaji,masoko nk.
3.Mtaji
Fedha za kugharamia shughuli zote kuanzia uandaaji wa shamba,uvunaji na utunzaji baada ya mavuno zipo?Fedha zinatakiwa ziwepo zote,maana unaweza kusema mwezi machi Mjomba atanikopesha fedha za mbolea halafu inafika machi Mjomba hana fedha na huna sehemu nyingine ya kupata fedha hapo mazao yatakosa mbolea na utapata hasara.
Haya hivyo haya ni mawazo yangu tu yanaweza yakawa siyo sahihi na pia ushauri huu umetokana na eneo nilipo.