Msaada: Napata choo chepesi na mwilibhukksa nguvu

D 2de A

Senior Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
183
Reaction score
32
Tafadhalini madokta naombeni msaada wenu wakaribu:

Jamani nina ndugu yangu wa kiume miaka 20 sasa, anasumbuliwa na tatizo lakupata choo chepesi/laini sio (kuendesha) yapata miezi 5 sasa tangia apatwe na tatizo hili..

Mara ya kwanza alianza kupata maumivu makali ya tumbo na kuendesha kwa siku moja then maumivu yale baada ya mwezi 1 yakawa yameisha ila akawa bado unapata choo chepesi sana(sio kuendesha) kinachovutika hata umwage maji bado sinki litabaki chafu hivyo hadi utumie brashi kukiondoa na anapoenda haja kubwa muda huo huo baada yakujisaidia huskia uchovu kama mtu aliyelala na mwanamke usiku kucha...

Wakati mwingine hujamba kijambo kinchonuka na tumbo kuunguruma kama anataka kuharisha lakini sio hivyo! tena...anasema ni mara chache sana hupata choo kigumu.

Pia anadai mara nyingine akila chakula kilichozidi mafuta kidogo tuu kesho yake huarisha nakukojoa mafuta(ute ute kam shahawa)

NB: Alishatembelea hospitali nyingi kubwa akapimwa na hata kupigwa x-ray but tatizo halikuonekana ndio maana nikaona nililete kwenu wadau ili tuweze kumsaidia huyu ndugu yetu kwani aajihisi discomfort sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…