Msaada: Napata discomfort upande wangu wa kushoto

ellyl

Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
85
Reaction score
127
Naomba mnisaidie wadau,

Mwaka jana nilipatwa na tatizo la shinikizo la juu la damu lakini wauguzi walinishauri na kuniambia ni tatizo la kupita hamna haja ya kutumia dawa za presa lakini kwa sasa ni takribani mwaka sasa kuna maumivu kwenye upande wangu wa kushoto.

Maumivu hayo huwa nayasikia kila ninapo jinyoosha au ninapo beba vitu vizito pia nikijaribu kuchokoza tatizo linaamsha dalili za presha huwa nahisi maumivu yanayo extend mpaka kwenye mkono na wakati mwingine hata shingo.

Pia nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku kula mlo kamili ila cha kushangaza tatizo lipo palepale naomba msaada kwa anayefahamu kuhusu hili tatizo.
 
Pole sana!
Kama uligundulika una tatizo la Presha (HTN) nafikiri ni muhimu ukalifuatilia kwa umakini sana!

Mtu anapokuwa na shinikizo la juu la damu/Presha (Hypertension, HTN) inabidi kuhudhuria clinic walau kila mwezi kwa ajili ya dawa, vipimo au hata kupata ushauri.

Matibabu ya Presha yamegawanyika ktk sehemu mbili:

(A). Kubadili mtindo wa maisha (life style modification). Hapa zingatia mazoezi na lishe ambapo tunashauri kuepuka chumvi nyingi sana kwenye chakula pamoja na kuacha pombe na sigara. Wakati unaendelea na hayo unapima Presha yako ili kuona kama inarudi kwenye kiwango cha kawaida .
(B). Kuanza kutumia dawa. Hii pale ambapo njia ya kwanza imeshindikana au kwa wale ambao tayari Presha iko juu na tayari wana dalili za hiyo shinikizo la juu la damu.

Kama mgonjwa yupo kwenye hatua mmojawapo hapo juu bado atalazimika kumuona daktari walau kila mwezi kwa ajili kuangalia maendeleo, asitumie tu dawa au kufanya tu mazoezi.

Kama bado unapata hizo dalili ni vyema ukafika kwa daktari MAPEMA SANA akuone na akushauri vizuri.
 
Unatakiwa kupata tiba haraka iwezekanavyo ili uondokane na hiyo hali,baada ya hapo ndiyo ufuate ushauri wa kanuni bora na mtindo sahihi wa afya yako.Huwezi kuugua malaria ukapona kwa kulala kwenye chandarua lazima kwanza utibu malaria iishe halafu uendelee kujikinga.
Uliliachia tatizo na hatimaye sasa limeanza kutengeneza tatizo jingine.Presha inapokuwa kubwa maana yake utendaji wa moyo unaathirika na wakati mwingine mishipa yake ama valve zinaweza kuathirika na madhara yake ndiyo hizo dalili unazozipitia.Tatizo hilo linapona kama utaamua kuwa serious kutafuta tiba.Kama utahitaji tiba na ushauri zaidi unaweza kuniuliza pia Mungu akuongoze.
 
Kuna wakati nipo vizuri kama mwezi wa nane nilikuwa nakimbia kila siku ila kwa sasa siwezi pia kuna muda nikikaa nasikia heart rhythm zinabadilika ghafla then na kuwa normal hii hali imenisumbua sana 😥
 
Kushoto Kuna moyo. Embu kafanye uchunguzi wa moyo. Achana na ushauri wa wauguzi kwanza.
 
Back
Top Bottom