Sasa sikia nikuambie Maumivu ya Kifua yanaweza kuwa yale yatokanayo na
1/ Moyo yaan Cardiac Chest Pain (CCP), haya kisababishi ni Moyo na kwakuwa ulipoenda tayari wame rule out possible cardiac causes Kwa Echo na ECG, ulitakiwa ufanye Vipimo vingine vinavyoangalia [emoji116][emoji116]
2/Yasiyotokana na Moyo yaan Non cardiac Chest Pain ( NCCP). Haya maumivu Mara nyingi husababishwa na Shida ya KOO LA CHAKULA na wengi huwa na shida ya Gastro-Oesophageal Reflux Disease (GERD), Ingawa pia matatizo haya ya NCCP yapo mbalimbali kama vile Msongo sugu wa mawazo, hypersensitivity kwenye Koo la Chakula, Maambukizi, Spasms n.k
Mara nyingi watu wenye Uzito mkubwa, wavuta sigara, pombe, watumishi sugu wa dawa za panado na NSAIDs ndio hupata sana shida hii ya maumivu ya NCCP.
Wagonjwa wengi hulalamika maumivu ya kuchoma, kama kitu kimekalizwa kifuani mwao, maumivu yanayosambaa kwenye shingo, bega la kushoto, mgongoni, kiungulia, Maumivu wakati wa kumeza na Ile hali ya kuwa anacheua cheua. N.k.
Kwa kusema hivyo ilipaswa hapo ulipopimwa ECG na Echo wakuunganishe kwa watu wa Gastroenterology ili waweze ku rule out NCCP.
Kwa lugha nyingine unatakiwa ufanyiwe
Oesophagoscopy
Oesopgageal manometry kuangalia motility yake
N.k kutegemea na watakavyofikia kwenye fikra zao za kitaalam kulingana na Dalili zako.
Wakati Huu, waweza nunua..
Antacid 10mls, unywe Kila baada ya Masaa 8 Kwa siku 5.
Vidonge aina ya Omeprazole 20mg unywe Kila Masaa 12 Asubuhi jioni ...... Fanya hivi Kwa siku 3-5, ukiona maumivu yanapungua basi una GERD.
Utarudi humu, unipe mrejesho, tuone hatua inayofuata!!.
HOSP NI MUHIMU, UENDE BABU!!.