Msaada: Nasikia kama kichomi fulani katika ya mapafu yaani kifuani

kalanga1

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
318
Reaction score
432
Mwenzenu kuna kitu kinaniuma lakini sijui ni nini, leo ni weak ya pili sasa, yaani kifuani katikati ya mapafu nasikia kama kichomi flani hivi.

Sijawahi kupata tatizo hilo tangu nizaliwe. Sasa juzi nipo ofisini nimekaa gafla kikaanza, kilianza kwa kasi kilikuwa kimenikamata haswaa, ikabidi nilale, kilinikamata kama siku 2, baadae kikaacha kwa muda, lakini sasa kimerudia tena.

Ila sasa hakiumi sana, but nikibeba mzigo nakisikia, nikipiga hata chafya nakisikia, nikijinyoosha pia nakisikia. Naomba msaada ni kitu gani hiki???

Na je nifanyaje ??? Plz nisaidieni jamani sina raha
 
Nenda hospitali kafanye check up kwanza
 
Ni maumivu kifuani upande wa kushoto?
 
Acha kutumia feni au punguza matumizi ya feni kwa muda hali itarejea kama kawaida
 
Acha kutumia feni au punguza matumizi ya feni kwa muda hali itarejea kama kawaida
umejuaje kama yuko sehemu ya joto? pengine yuko Mbeya, Iringa au hata Ulaya ambako kwa sasa ni barid la kufa mtu!
 
umejuaje kama yuko sehemu ya joto? pengine yuko Mbeya, Iringa au hata Ulaya ambako kwa sasa ni barid la kufa mtu!

Nimeongelea experience mkuu. Watu wengi ambao wana matatizo hayo chanzo kikubwa huwa ni matumizi ya feni
 
katatizo kadogo tu haka mkuu, ila ndio hivyo mambo ya kushautiana dawa hapa bila vipimo si nzuri sana.
Kapime kwanza then mengine yatafuata, hata ECHO tu inatosha.
Jali afya yako,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…