Msaada: Nasumbuliwa na Acid tumboni

Msaada: Nasumbuliwa na Acid tumboni

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
1,312
Reaction score
944
Habari wataalamu, huwa nasumbuliwa sana na Acid tumboni hivyo kusababisha kujisikia hali ya tumbo kuwaka moto, mwaka jana mwanzoni kuna mtu alinishauri nitumie dawa fulani inaitwa Ranitidine Lakini nasikia hii dawa imezuiliwa. Nilikuwa naomba msaada mbadala wa hii dawa tafadhali
 
Aisee hili tatizo naona lishakuwa common sana kwa sasa, kuna jamaa hapa ofcn wawili wameshaambiwa hvyo na wamepewa list ya vyakula vya kutokula.

Kuna cousin wangu ndo amepata shida sana imesababisha changamoto ya figo. Na imegunduliwa late.

Nakushauri pita maeneo ya posta ya zamani krb na kituo cha mwendokasi cha city kuna hospt inaitwa polylicnic nasikia wanajitahidi kukabiliana na changamoto kama hizo.
 
1 Kama nimpenzi wa kachumbali acha kabisa
2 Usile kuvimbiwa,kula chakula kidogo.
3.Usimalize kula alafu ukaenda kulala,tembea au simama kwa muda kidogo
 
Habari wataalamu, huwa nasumbuliwa sana na Acid tumboni hivyo kusababisha kujisikia hali ya tumbo kuwaka moto, mwaka jana mwanzoni kuna mtu alinishauri nitumie dawa fulani inaitwa Ranitidine Lakini nasikia hii dawa imezuiliwa. Nilikuwa naomba msaada mbadala wa hii dawa tafadhali
Mkuu pole sana dawa zipo za kuondosha Asidi mwilini mwako Dawa za Asili ukitumia utaweza kupona.
 
Habari wataalamu, huwa nasumbuliwa sana na Acid tumboni hivyo kusababisha kujisikia hali ya tumbo kuwaka moto, mwaka jana mwanzoni kuna mtu alinishauri nitumie dawa fulani inaitwa Ranitidine Lakini nasikia hii dawa imezuiliwa. Nilikuwa naomba msaada mbadala wa hii dawa tafadhali
Jaribu kutumia Omeprazole 1x2 kabla ya kula kwa mwezi mmoja
 
Nlikua na tatizo hill.nkawa kila asubuhi nachukua glass au kikombe ujazo wa kama robo Lita.naweka maji ya moto sana.nachukia limao naliosha bila kumenya,nakata slesi nyembamba nadumbukiza kwenye ile glasi unzaivha kwenye Yale maji kwa kama dakika kumi kisha unaanza kunywa taratibu maji yakiwa na joto la kawaida.

Unafanya hivi kabala hujala chochote.na ukae kama nusu saa ndio ule .ni asubuhi tu
 
Ki ukweli acid inasumbua sana

Tumia dawa aina ya omeprazole kwa muda wa mwezi mmoja

Acha kula vyakula vinavyoleta kiungulia kama vile maharage, dagaa,viazi vitanu, viporo na makachumbari..

Mwenyewe ndo nipo kwenye doz wiki ya 2 sasa ila naona nafuu kidogo
 
Aisee kwangu nahisi ishakuwa chronic gesi inatoka tumboni na kuniunguza sehemu za Koo la chakula

Ngoja nikimbilie hospital faster
 
Ni vyema kuwapa nafasi wataalam wa afya kwani mambo mengine hufanana sana. Mfano wa hiki unachojaribu kukieleza kinaweza kuwa acid reflux.
Hivyo, watu huweza kuwa na:
1: Shida ya acid nying na gesi
2: Acid reflux
3: Vijiwe kwenye kwenye mfuko wa nyongo

Dalili hufanana kwa kiasi na tiba hufanana kwa kiasi. Lakini kuna mambo ya kuzingatia ambayo ni tofauti kidogo kulingana na tatizo.

Hivyo, unaweza kutumia dawa ukaona huponi kumbe tatizo lako ni tofauti na mwenzako.
 
Asante Sana, hapa kesho tu natinga hospital mapema kabisa
 
Habari...mi nasumbuliwa na mgongo Kama unawaka Moto sehemu za mabegani lakin pia mdomoni Kuna hali ya uchungu chungu na hapa sehem ya Koo kun mda Kama Kuna kitu flani hiv na mda mwingine panakauka
 
Daaah mku ulipata dawa mana dalili zote hizo ninazo
 
Habari wataalamu, huwa nasumbuliwa sana na Acid tumboni hivyo kusababisha kujisikia hali ya tumbo kuwaka moto, mwaka jana mwanzoni kuna mtu alinishauri nitumie dawa fulani inaitwa Ranitidine Lakini nasikia hii dawa imezuiliwa. Nilikuwa naomba msaada mbadala wa hii dawa tafadhali
Pole Sana.Jaribu kutumia mbegu za unga WA parachichi zinaweza kusaidia.
 
Back
Top Bottom