Msaada, nasumbuliwa na U. T. I

Msaada, nasumbuliwa na U. T. I

Brotha man

Member
Joined
May 26, 2018
Posts
10
Reaction score
3
Nasumbuliwa na u.t.i mda mrefu pia nmetibu na dawa nyingi inarud hvi tatzo ni nini?
 
jibu ni

tafuta hospital kubwa kwa ajiri ya kufanya urine culture kipmo cha kuotesha wadudu waliopo ktk mkojo na kuwaingizia dawa drug sensibility test kwa ajir ya kutambua dawa hipi ni susceptible au yeny nguw kwa wakat huo

Hichii kipimo nii sh ngap samahani
 
Nasumbuliwa na u.t.i mda mrefu pia nmetibu na dawa nyingi inarud hvi tatzo ni nini?

UGONJWA WA URINTI/UARY TRACT INFECTION

Ugonjwa wa UTI ni nini?


UTI kitaalamu ni “Urinary Tract Infection” ni magonjwa au maambukizi yanayoathiri mfumo wa kutengeneza na kutoa mkojo nje ya mwili. Mfumo huu unahusisha kibofu cha mkoja, figo pamoja na milija inayounganisha kibofu cha mkoja na figo. Pindi wadudu yaani bacteria wanapoingia katika mfumo huu wanaweza kusababisha maambukizi ambayo mara nyingi wataalamu hupenda kuyaita UTI.

Mara nyingi maambukizi ya mfumo huu wa mkojo huwa ni maambukizi ya kibofu cha mkojo (Bladder infections). Maambukizi ya kibofu cha mkojo kawaida hayana madhara makubwa kama yakitibiwa haraka. Yasipotibiwa yanaweza kusambaa hadi kwenye figo zako. Maambukizi ya figo yana madhara makubwa sana kwani huaribu figo ambapo unaweza kupata magonjwa ya figo ambayo tunayaita Kidney au Renal Deseases.

Nini usababisha UTI?

Kawaida Bakteria uingia kwenye mfumo wako wa mkojo kupitia kwenye mlija mdogo wa mkojo ujulikanao kitaalamu kama urethra mlija unayobeba mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo kwenda nje ya mwili. Bakteria wanaosababisha maambukizi uishi katika utumbo mkubwa wa chakula na upatikana kwenye choo au kinyesi. Mara nyingi bacteria hawa wanaitwa E. Coli. Bakteria hawa upitia kwenye urethra na kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye figo na kusababisha maambukizi.

Wanawake hupata UTI zaidi ya wanaume kwa sababu milija yao ya kutoa mkojo kwenye kibofu cha mkojo ni fupi zaidi ya wanaume na hivyo kuwezesha bacteria kusafiri kwa urahisi zaidi hadi kwenye kibofu cha mkojo. Pia kufanya tendo la ndoa au kujamiana pia kuna rahisisha bacteria kuingia kwenye urethra.

Pia unaweza kupata UTI kwa kutokunywa maji ya kutosha kwani maji husaidia kutengeneza mkojo wa kutosha na hivyo unapokojoa unasafisha milija yako ya kutoa mkojo nje ya mwili.

Pia watu wenye ugonjwa wa kisukari wana hatari ya kupata UTI mara kwa mara kwani kinga ya mwili hushuka na hivyo kusaidia kupata maambukizi kirahisi na pia mkojo anaotoa huwa na kiasi kikubwa cha sukari ambacho husaidia wadudu kukua vizuri. Pia mama mjamzito hupatwa na UTI zaidi. Uwezekano wa kupata maambukizi ni makubwa endapo unatatizo linalosababisha mkojo kushindwa kutoka nje ya mwili kama vile, mawe kwenye figo yaani kidney stones au ongezeko la tezi la kibofu cha mkojo yaan enlarged prostate kitaalamu BPH.

Wanawake upata UTI mara kwa mara na hizi zinaweza kuwa sababu zinazoongeza uwezekano wa kupata UTI mara kwa mara:

Usafi wakati wa kujitawaza wakati wa haja kubwa; baadhi ya wanawake hupenda kufuga kucha ndefu kwa ajili ya urebo hivyo wakiwa na haja kubwa uogopa kugusa choo hivyo ujimwagia maji ambayo yanaweza kupiga vipande vya choo hadi kwenda kwenye njia yao ya mkojo na hivyo kuweza kupata maambukizi. Pia wengine ujitawaza kwa kuelekea njia ya ukeni hivyo kuongeza nafasi za kupata maambukizi.

Choo chafu: Vyoo vya watu wengi vya kukalia pia ni chanzo za kusababisha maambukizi.

Taulo za kuogea na nguo za ndani

Kufanya tendo la ndoa kinyume na maubile

Kusafisha ukeni na sabuni hususan sabuni ambazo ni medicated kama delto kwani uondoa kinga za sehemu husika (normal flora).

Dalili za UTI

Kujisikia maumivi au kuwashwa wakati wa kukojoa

Kujihisi haja ya kukojoa lakini unapoenda kukojoa mkojo hautoki wa kutosha badala yake unatoka kidogo

Tumbo kulihisi kubwa au zito

Mkojo kutoa harufu mbaya au mkojo kuwa kama wingu

Kupata maumivi mgongoni hususani chini ya mbavu haya ni maambukizi ya figo

Kupata homa na kutetemeka

Kichefuchefu na kutapika

Matibabu: Kunywa Maji ya Madafu,Maji ya Miwa Maji ya Matikiti Maji kwa wingi kunywa Maji ya kunywa kwa siku kunywa maji lita 3 utaweza kupona. Ukitaka kupona haraka nitafute nipate kukutibia kwa siku 14 utapona maradhi yako na kusahau kama ulikuwa unayo hayo maradhi ya UTI.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu

UTI.jpg
 
Back
Top Bottom