Msaada natafuta kazi/ajira

Msaada natafuta kazi/ajira

Hot27

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2020
Posts
372
Reaction score
691
Habari wanajukwaa

Mimi ni kijana wa miaka 23
Jina ni Rajab
Makazi ni Kwa Aziz Ali, Dar es salaam
Elimu nimesoma hadi kidato cha sita kisha nikaenda chuo.
Nimehitimu chuo mwaka huu (Lakini sitaweza pata cheti wala kufanya mahafali hadi mwakani juu ya changamoto zilizonitokea ikasababisha mitihani miwili niikose).

Nimekuja kwenu wanajukwaa kupata usaidizi wa kazi ama ajira yoyote. Mimi ni kijana muaminifu, mtiifu na mwenye bidii. Nina afya thabiti na mafunzo ya JKT yamenijenga kuwa muajibikaji na kuweza kuendana na mazingira ya kazi.
Nina uwezo wa kusoma na kuzungumza kwa ufasaha Kiswahili na Kingereza, nina ujuzi wa kutumia kompyuta, kufanya mahesabu ya kawaida, kusimamia na kuendesha mitandao ya kijamii, nina ujuzi na mambo ya habari (ndicho nilichosomea).

Ombi langu ni kazi yoyote hata ya nje ya taaluma (isiyohitaji taaluma) nipo tayari kufanya tena kwa ustadi wa hali ya juu.

Naomba kuwasilisha kwenu wana JamiiForums, Mungu awatangulie na nina imani nitapata usaidizi pia nipo tayari kujibu kila nitakachoulizwa eidha hapa ama PM
Mawasiliano yangu ni 0682 115 568
AHSANTENI
 
Back
Top Bottom