Msaada: Natafuta kazi au kujitolea ya Assistance accountant

Msaada: Natafuta kazi au kujitolea ya Assistance accountant

AfricaUnited

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2010
Posts
2,367
Reaction score
1,293
Habari wana jamvi.

Nina mtoto wa dada wa kiume anamiaka 28 , amemaliza degree ya accountancy mwaka 2017 , nilimuingiza kwenye biashara , sasa anataka pata ajira biashara ngumu.

Hana uzoefu wa kazi ya uhasibu yoyote ,ila ni muelewa wa haraka na yupo tayari kujitolea mkoa wowote tanzania.

Nitashukuru kwa msaada.
 
Kuna wale kwa hisani ya watu wa Marekani walikua wanachukua sana Accountants sijui bado wapo...

Cc: mahondaw
 
Mtoto wa dada
Ana miaka 28
Kamaliza degree 2017

Lakini hana gutts wala uthubutu wa kuja kwenye forums kama hizi kuomba ama kutafuta mwenyewe kazi.

Anatuma mtu aje amuombee yeye aweze kuingia tu..asipojua ugumu wa kupata kazi ataithamini kazi???

Raha ya mtu kutafuta kazi mwenyewe na kuipata ni kwamba hata yakitokea mapito mbalimbali na changamoto ofisini utakapokuwemo utayashinda.

Lakini hizi kazi unatafutiwa na mjomba wakati wewe una miaka 28 ndo inafanya vijana wajilegeze sana.

Kwa maelezo yako inaonekana hata kijana hana alilowahi kufanya ukiachia mbali kumaliza degree...maana hata biashara unasema "ulimwingiza"....

Na naamini kabisa mpaka kamaliza degree ni hela ya wazazi na walezi imetumika hajawahi fanya vibarua kujisomesha...na ndo mana mnapambana sana kuhakikisha mmemsomesha na anapata kazi.....ushauri wangu mwinginzeni kwenye changamoto za ajira na yeye apambane...jitu la miaka 28 ni kubwa mno.
 
Mwambie aende ofisi za TAESA huko ndipo wanaombeaga wahitimu sehemubza kujitolea kwenye mashirika.

Nina ndugu yangu naw alimaliza hio kozi ya accounting mwaka 2017 alipangiwa kujitolea TRA analipwa laki 3 kila mwezi.
 
Habari wana jamvi.

Nina mtoto wa dada wa kiume anamiaka 28 , amemaliza degree ya accountancy mwaka 2017 , nilimuingiza kwenye biashara , sasa anataka pata ajira biashara ngumu.

Hana uzoefu wa kazi ya uhasibu yoyote ,ila ni muelewa wa haraka na yupo tayari kujitolea mkoa wowote tanzania.

Nitashukuru kwa msaada.
Haujaweka namba ya simu
 
Back
Top Bottom