Habari wakuu!
Natafuta milioni tatu (3,000,000) kwa ajili ya kuanzisha biashara ya ufugaji kuku wa nyama (Bloilers). Nimeamua kuanzia na mtaji mdogo ili nijifunze changamoto za biashara hii na jinsi ya kupata faida.
Nimeshauriwa kuwa biashara hii inalipa sana tena kwa muda mfupi hata ndani ya mwezi mmoja. Nitashukuru pia kama nitapata mchanganuo wa gharama kwa kuanzia na kuku 700. Banda nitakodi.
Kimsingi natafuta wapi nitapata mkopo wa Tsh 3m niweze kurun biashara hii. Nimetembelea kwenye benki ya Akiba wanahitaji biashara inayorun tayari ili wanipe mkopo kwahiyo nimeshindwa. Nina kiwanja na boma lililokamilika hadi hatua ya kupauliwa kama security.
Mawazo yenu nitayathamini sana ili niweze kujiajili. Kazi za kuajiliwa ni ngumu sana kupata. Kama unashauri binafsi pia unaweza kunipm, Nipo serious wakuu!