Msaada: Nataka kuanza biashara ya daladala

sir venance

Senior Member
Joined
Oct 26, 2017
Posts
151
Reaction score
223
Nahitaji kununua gari ya biashara aina ya coster, najua kuna wajuzi wa haya mambo nahitaji kufahamu gharama za uendeshaji wa hii biashara, itanilipa baada ya muda gani, na hasara zake ni zipi, nipo dar na biashara nahitaji kuifanyia hapa hapa, karibuni.
 
Mimi sio mjuaji sana wa huo upande ila ninaweza kukupa tu ushauri wa mwanzo!

Biashara ya Daladala ni moja kati ya biashara ambazo zinalipa na kuinua sana kipato. Kwa kifupi ni biashara nzuri sana ukiwa na nidhamu nayo. Na ndio maana leo, unaona kuna utitiri wa magari na hata serikali nayo ikaamua kuweka magari yao!

Gharama za uendeshaji bila shaka zinategemeana sana na wapi gari lako litakua linakwenda, na hali ya barabara hio na masaa ambayo gari litakua likitumika.

Hasara kubwa ipo kwenye upande wa madereva na makonda, hao ndio pasua kichwa ilipo, nakushauri kama una ndugu yako wa karibu, ukamuweka akasimamia upande huo wa "ukonda" maana hii style wamiliki wengi wa madaladala (haswa wachagga) ndio hua wanafanya sana.

Again:

Uzoefu wangu mkubwa upo kwenye uuzaji magari haya ya abiria, ila sio kwenye biashara hii ya kubeba abiria.

Kwahio, niliyoyatoa ni maoni yangu, na niko tayari kusahihishwa.


Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…