Msaada: Nataka kuanzisha biashara itakayokua mbeleni

Stv Mkn

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
328
Reaction score
273
Habari zenu wadau,

Mimi najitokeza ninahitaji ushauri kutoka kwenu wa kibiashara. Nina nia ya kuanzisha biashara ya nguo sababu binafsi napenda mavazi na nina jicho la kuona vitu vizuri.

Katika utafiti wangu sehemu mbalimbali hapa Dsm nimegundua sehemu inayolipa vizuri ni kariakoo hapa nguo zinanunuliwa sana haswa za kina dada na nguo zinazonunuliwa haswa ni za kati sio classic sana wala sio midosho sana, pia nguo za ndani ni dili sana kkoo.

Pia nimegundua hapo hapo kariakoo vifaa vya simu navyo ni biashara nzuri sana na mbagala rangi tatu.

Changamoto yangu pamoja na kuwa na nia ya kufanya biashara hili eneo ni mtaji kwani flemu hapa ni ghali sana, na kwa level yangu siwezi kupangisha flemu hivyo nilitafuta ata uchochoro nikapata ila nao ni pesa ndefu wanaitaji laki 3 kwa mwezi unalipa miezi 12 na dalali laki 3...so ni kama milion 4 kupata kijieneo tu cha kuweka bidhaa.

Nia yangu hipo palepale lazima nifanye biashara hapo kkoo ata kama sio leo.

Nachoomba mnishauri ni kitu kimoja kwa sasa nina mtaji wa laki 6 ninataka kuukuza ufikie level za kufanya biashara kkoo. Mipango yangu ni kuanza na biashara ya kufata nguo Uganda au Kenya nimepata taarifa huko kuna nguo nzuri kwa bei nzuri nataka. kuja kuuza hapa bongo, tatizo langu ni wateja wa kuniweZesha biashara yangu kuzunguka kwa haraka nitawapataje sababu kwa mtaji wangu siwezi kuanzisha flemu na kumwaga biashara chini kkoo au karume ni risk sana wagambo wakikuotea utapoteza kila kitu.

Kwa hiyo nachotaka ni hilo tu, kuanzisha biashara ya mavazi eg nguo pochi viatu sasa nitapataje wateja kirahisi?? Nitawafikiaje hao wateja....?? nisaidieni ushauri wadau.

Waione pia. Matanzia kizebazeba masai dada Money Stunna wiseboy CYBERTEQ josefast Mr.Busta charminglady Dumelang Mathematician Zanzibar Spices na wadau wote hapa jf.
 
Last edited by a moderator:
Tumia simu yako kutafuta wateja, ongea na wenye maduka wasiyoweza kusafiri alafu uwe unawapelekea Kwa bei ya jumla.
 
mtaji mdogo sana huo........nguo za uganda mitumba ndo ipo na kwa mtaji huo SIO LAZIMA UUZE NGUO KWANZA MAANA NI MDOGO KUNA KITU CHA KUFANYA UUKUZE

LAKINI KAMA UTATAKA NGUO TU REPLY THEN NIKUAMBIE UENDE WAPI
 
Tumia simu yako kutafuta wateja, ongea na wenye maduka wasiyoweza kusafiri alafu uwe unawapelekea Kwa bei ya jumla.

Asante kwa mawazo mazuri.Mungu akubariki.
 
mtaji mdogo sana huo........nguo za uganda mitumba ndo ipo na kwa mtaji huo SIO LAZIMA UUZE NGUO KWANZA MAANA NI MDOGO KUNA KITU CHA KUFANYA UUKUZE

LAKINI KAMA UTATAKA NGUO TU REPLY THEN NIKUAMBIE UENDE WAPI

Yap nakubaliana na wewe kamtaji bado kadogo. Naomba uniambie vyote vyote nifanyeje niukuze mtaji. Pia hiyo sehemu ya kwenda na huu mtaji kwa nguo.
 
baadaye unitafute unijuze zaidi hii habari!!!
 
Yap nakubaliana na wewe kamtaji bado kadogo. Naomba uniambie vyote vyote nifanyeje niukuze mtaji. Pia hiyo sehemu ya kwenda na huu mtaji kwa nguo.

vyote vyote?
lazima ufanye kimoja
either ununue nguo za special dar upeleke mkoani na hii kwa mtaji huo itabidi mkoani uuze reja reja na kwa pesa hiyo lazima uwe na mtu wa kukuuzia huko mkoani
HII ITAKUSAIDIA KUPATA UZOEFU KWA KUJUA MADUKA NA PIA KUJUA WENZAKO WANAFANYA VIPI BIASHARA

pili KAMA BADO UNATAKA NGUO
chalenji ni wapi pa kuuzia kwa dar unaweza nunua balo la mtumba unaoanzia laki 2 mpaka 1 na nusu inategemea nguo za aina gani sehem ya kununulia ipo CHANGAMOTO NI WAPI UTAKIWEKA KIJIWE CHAKO??????

bado unataka nguo???
 
Ndio dadaa bado nataka nguo, nakufatilia kwa makini maelezo yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…