Msaada: Nataka kufungua Duka la Madawa Baridi ya Binadamu (Pharmacy)

bigcell

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
219
Reaction score
60
Wana Jf poleni na majukumu mbalimbali ktk ujenzi wa Tz yetu.

Mimi nilikuwa muajiriwa wa serikali ktk Idara ya Afya. Nimekuwa ktk ajira kwa kipindi kirefu zaidi ya miaka 20, serikalini na nimefanya kazi kwa uadilifu mzuri bila ya kuwa na kashfa yeyote ile. Baada ya kuona maisha yanakwenda sina maendeleo yoyote nimeona niombe kustaafu kwa hiari nilipwe changu nikaanze maisha kujiajiri kupitia fani yangu ya famasia. Kiukweli umri wangu bado ni mdogo hivyo nimeonelea nichukue maamuzi magumu ya kuanza maisha mapya ya kujiajiri.

Nina mtaji wa tsh. 20miln. ambazo nilizipata kwa kuuza ka plot kangu huko kimbiji maana niliona sitaweza kuliendeleza kutokana na mshahara kuwa mdogo na majukumu niliyonayo.

Sasa Wadau najua humu ndani kuna wajasiriamali wengi na wanauchumi wengi naombeni mawazo yenu na ushauri wenu jinsi gani nijikwamue.

Nawakilisha.
 
Are you a pharmacist by proffessional?Amma umekuwa katika kada ipi in a health sector?
 
pitia jukwaa la uchumi na biashara kuna thread kama yako.....watu wametoa kila aina ya ushauri unaotakiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…