Msaada:Nataka kwenda Burundi au Comoro kwa ajili ya kutembea tu.

Msaada:Nataka kwenda Burundi au Comoro kwa ajili ya kutembea tu.

Titans

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,459
Reaction score
3,369
Habari wana ChitChat,

Natumai mu-wazima wa afya, nina mpango wa kwenda Bujumbura kwa ajili ya kutembea tu, nilikuwa napenda kufahamu je hoteli gani ni cheap pale Bujumbura iliyo karibu na Ziwa Tanganyika? na bei ina-range kiasi gani? napanga kwenda na basi je nauli ina-range how much? je kwa ujumla maisha ya Bujumbura ni ghali kiasi gani?

nimefanya utafiti kupitia internet lakini kuna 5 star hotel tu zilizo gharama sana labda kuna watu wanajua humu mbadala.

Option ya pili.

Au ningependa kwenda Comoro mji wa Moroni, nimesikia kuna beach nzuri sana kule, kwa ambaye amefika je gharama za hoteli zikoje? na visa inakuwaje? nataka kwenda kwa boat ya mizigo kutokea dar maana ndege ni gharama sana sitaweza ku-afford.

Msaada please.
 
Back
Top Bottom