Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
Huu ugonjwa wa ngozi umenisumbua sana umenipata mgongoni,nimetumia dawa za kila aina kwanzia fluconazole za kumeza hadi gentrisone za kupaka hauishii na bado unanirudia,je nautibuje wadau? au namuona mtaalam gani anisadie?
pole sana ndg mischa, nakushauri uende pale Manzese kwenye pharmarcy ya FABEK juu ghorani uliza daktari wa magonjwa ya ngozi huwa anapatikana hapo kila Jumatatu saa 10 jioni. Kama hutafanikiwa uje ulete mrejesho
![]()
Huu ugonjwa wa ngozi umenisumbua sana umenipata mgongoni,nimetumia dawa za kila aina kwanzia fluconazole za kumeza hadi gentrisone za kupaka hauishii na bado unanirudia,je nautibuje wadau? au namuona mtaalam gani anisadie?
Mkuu.@mischa Ingelikuwa Bora uende Hospitali kupima na kujuwa una ugonjwa gani wa ngozi kuliko kutuonyesha hiyo tu picha haitosaidia kitu ili tuweze kukusaidia kukupa ushauri ni nini cha kufanya mimi nina hisi kwa uzoefu wangu utakuwa huo ugonjwa wako ni huu hapa chini unaitwa kwa jina MKANDA WA JESHI (HERPES ZOSTER/SHINGLES)
![]()
Kwa takribani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa, ugonjwa huu ni dalili ya wazi kabisa ya mtu kuwa na VVU, imani ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa
majina ya kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali .
Visababishi
Kama tulivyokwisha tangulia kueleza hapo juu, ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva
fulani za mwili. Baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi.Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia.
Vihatarishi
Mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:
Wenye umri wa zaidi ya miaka 60
Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja
Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo.
Je mkanda wa jeshi huambukizwa?
Hapana ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine! Lakini iwapo itatokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga maishani mwake na ambaye pia hajawahi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo akakutana na mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto au mtu huyo atapatwa na ugonjwa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.![]()
Dalili
Dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yakiambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi. Maumivu pamoja na hisia za kuungua huwa makali sana na hutokea kabla ya vipele/michubuko kutokea kwenye ngozi.
Kawaida, vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, mdomo au masikio.Dalili nyingine ni pamoja na :
Maumivu ya tumbo
Homa
Maumivu ya mwili mzima
Vidonda sehemu za siri
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya viungo
Kuvimba kwa mitoki/ matezi
Iwapo neva za maeneo ya uso zitaathiriwa, mgonjwa anaweza kupatwa na matatizo ya kuona, kuonja, au kusikia.
Vipimo
Ni nadra sana kufanya Vipimo maalum kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuchukua historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa.
Vipimo vya damu yaani FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu na antibodies dhidi ya virus wa tetekuwanga.
Matibabu
Matibabu ya mkanda wa jeshi hujumuisha matumizi ya dawa kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virus wanaosababisha ugonwja huu.
Nimeipenda hii ya kumshauri aende hospital, ningekuwa natumia pc ningekupa like.
hiyo picha ni kama psoarisis,ila kama ni eczema, unasababishwa na allergy,na cha muhimu uangalie vyakula unavyokula,ni vizuri ukafanyiwa allergy test,kujua kitu gani kinakudhuru.vile vile ni vizuri uvae nguo za aina ya cotton,na sabuni za kuogea utumie zisizo na ma chemical.ukifata masharti huwa inasaidia.maana ugonjwa huo,unaweza ukajiona umepona,baadae ngozi inaharibika tena,ila kuna mafuta fulani yanaitwa lookman hayat tel,jaribu kuyatafuta maduka ya wahindi maybe na maduka ya waarabu ni mazuri mno,google utayaona yalivyo.niliambiwa unaitwa eczema
nashukuru ntayatafuta haya mafuta cjui hapa dar naweza yapata wapi?hiyo picha ni kama psoarisis,ila kama ni eczema, unasababishwa na allergy,na cha muhimu uangalie vyakula unavyokula,ni vizuri ukafanyiwa allergy test,kujua kitu gani kinakudhuru.vile vile ni vizuri uvae nguo za aina ya cotton,na sabuni za kuogea utumie zisizo na ma chemical.ukifata masharti huwa inasaidia.maana ugonjwa huo,unaweza ukajiona umepona,baadae ngozi inaharibika tena,ila kuna mafuta fulani yanaitwa lookman hayat tel,jaribu kuyatafuta maduka ya wahindi maybe na maduka ya waarabu ni mazuri mno,google utayaona yalivyo.
jaribu maduka ya wahindi yoyote yale. au hata maduka ya madawa,maana hiyo dawa ni from india inasaidia sananashukuru ntayatafuta haya mafuta cjui hapa dar naweza yapata wapi?