Msaada: NatWest Financial services

Msaada: NatWest Financial services

ze encyclopedia

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
316
Reaction score
180
Habari wana jf
Mimi no mjasiriamali ninaemiliki ka daladala kamoja hapa jijini. Katika harakati zangu za kuongeza mtaji nilipata kipeperushi cha hiyo kampuni tajwa hapo juu kwamba wanatoa mikopo bila dhamana. Nami sikusita nikasogea ofisini kwao IT plaza posta.
Cha ajabu
1. Niliwaambia nahitaji kuongeza daladala
mbili tu....wao wakakataaa....wakasema
watanikopesha daladala 50.
2. Tena wataniongezea na 20% fund ya
mkopo nitakaochukua kama working
capital ya kuanzia biashara hiyo. Yaan
mfano daladala ziligarimu laki moja
nitapewa ziada 20% ya laki. That is
20,000/=
3.wanachotaka nitoe dola elfu tatu tu kama subscription fees.
KILICHONISHTUA
Wanasema pesa zinatoka nje...ila ukimuuliza wapi hasa hana majibu...
Anasema guarantor ni bima.ukimuuliza bima gani hatoi majibu.....
WADAU NAOMBA MSAADA KWA ANAEWAJUA WATU HAWA NISIJE LIWA NA HIKI KIDOGO NILICHONACHO. NIKWELI WANATOA MIKOPO MINONO HIVYO?
NAWAKILISHA
 
Back
Top Bottom