Jamani naombeni msaada wa kisheria na hata ushauri. Nataka kuoa mtoto mmoja wa Kiunguja ila wazazi wake na familia yake haitaki kwasababu mi natoka Bara na pia ngozi yangu nyeusi (huyo mtoto ni mwarabu). Sasa wameanza juhudi za kumtafutia Mume.
Huyo mtoto yuko tayari kutoroka kuja kuishi na mimi, sasa nataka kujua kama naweza kumuoa bila idhini ya wazazi wake au ndugu maana hakuna njia nyingine na ameniambia ikishindakana basi yeye bora atangulie kaburini kuliko kuolewa na Babu mwenye wake wanne.
Kwa taarifa mimi ni muislam.
Mwenzenu katika Mashaka
Fiksi.
Sijawahi ndo nataka kuanza maisha mkuu. Na sio siri nampenda sana huyo mtoto niko tayari kwa lolote ilimradi awe mke wangu

mkuu fiksi vipi yule unaye-share na jini! umemuacha au ndio huyu huyu? kwa hiyo umefanikiwa kumthibiti yule jini!?
mpe mimba then wazazi wataridhia tuu
kwa vile nyinyi ndio mtakao ishi pamoja na kukabiliana na ndoa yenyu wakati wote wa raha na shida basi wao hawana huwezi wa kusimamisha ndoa yenu.kwahio kusiwe kipingamizi kabisa fanya mpango mtoto aje bara umuoe muishi pamoja na mungu hawajalie ndoa yenu hidumu na hawaepushe na matatizo yoyote ambayo ndugu zake wataleta.kila kheri muheshimiwa .
Hakuna ndoa isiyokuwa na baraka za wazazi ikadumu kuwa serious man