Nahic watakuwa hawajauelewa ila niule ule
Kiongozi Suala si kutokuuelewa, Suala ni kwamba:-
Kama ule Uzi usingefutwa ningekuwekea hapa na kisha tungepima Mizani, nnakuahidi hata wewe mwenyewe Muhusika Mkuu ungeona tofauti.
Unajua kwanini?
Hapa umezungumzia kuwa Ndugu yako anasumbuliwa na matatizo ya kuvimba Mwilini mwake, ikiwemo na viungo vyake pamoja na maumivu makali.
Uzi uliofutwa ulidai Ndugu yako anasumbuliwa na Minyoo na mkaenda Hospitali mkapewa Dawa za Minyoo, baada ya Ndugu yako kuzitumia hizo Dawa za minyoo tu akaanza kuvimba.
Tukiweka Mizani, jibu ni kwamba:-
Kwa Uzi huu Ndugu yako tatizo la Kuvimba Mwili wake ni la kwaida, amma naweza sema ni Desturi yake Kuvimba Mwili, au naweza sema, ni Ugonjwa unaomsumbua mara kwa mara, nikiwa na maana Ugonjwa huo wa kuvimba haujaanza jana wala leo.
Tukija kwenye Uzi wako uliofutwa SIASA, ni kwamba:-
Ndugu yako alipatwa na Minyoo, mkampeleka Hospitali, akapewa Dawa, na mara baada ya kupewa Dawa ya Minyoo tu, matokeo yake Mwili wake ukaanza kuvimba. Na ukiangalia jibu unapata tatizo la yeye kuvimba Mwili limesababishwa na hizo Dawa alizopewa Hospitalini.
Je hapo kuna mwingiliano wowote wa Mabandiko yako yote mawili?
Je hapo utawalaumu Viongozi waliofuta Uzi wako?
Jibu ni kwamba ingekuwa Uzi wako huu unamwingiliano na Uzi wako ule uliofutwa SIASA, pasi na kipangimizi chochote kile Uzi wako ule uliofutwa SIASA na Uzi wako huu ungeunganishwa.
Kwa haraka haraka umeshindwa/unashindwa kufikiria kitu kama hiki!
Hivi hizo Shule mlienda kusomea ujinga? (Kwa Sauti ya Bibie FAIZA)