Msaada: Ng'ombe wangu anaweza kufa

Andresen

Member
Joined
Feb 21, 2019
Posts
50
Reaction score
105
Ndugu zangu,

Ng'ombe wangu amezaa mwezi December, 2018. Lakini toka amezaa hali yake imekuwa sio kabisa. Anakula sana tena sana lakini anazidi kukonda kila siku na sasa amebaki mifupa tu na hali inazidi kuwa mbaya kwake.....ANGALIA PICHA YAKE HAPA CHINI.

Pia alipozaa mtoto mwezi December nilimwita mtaalamu alimchoma sindano, na baada ya mwezi alirudia kumchoma tena sindano akidai sasa atakuwa na afya nzuri lakini hali ndio imekuwa hivyo.

Kuna watu wameniambia huenda atakuwa na ugonjwa wa konokono wa kwenye maini, je inaweza kuwa ni kweli? Na kama ni kweli, je wataalamu wa mifugo mnashauri nitumie dawa gani ili kuweza kumnusuru huyu ng'ombe wangu?

Naombeni msaada wenu wa dawa sahihi kulingana na uzoefu na utaalamu wenu. Angalia picha yake hii hapa

 
Mimi nilijua ng’ombe yule mwingine
 
Watu kama mazuzu vile, hakuna yeyote ambaye amesaidia mpaka hapa
 
Watafuta madaktari hata watatu tofauti,pole sana
 
Kwa kumtazama tuu anaonekana anatatizo kubwa la minyoo, hapo mtafute mtaalamu ili amchome sindano za minyoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…