Wakuu tafadhali mwenye uzoefu na masuala ya ufugaji nguruwe wanakaribia miezi 5 lakini bado kasi sio nzuri ya ukuaji kwa waliowaona utahisi wa miezi 3 na nusu tatizo nini. NB naishi maeneo yenywe baridi chini ya centigrade 20 kwa wastani.
Lakini Kuna mitaa mingine nguruwe wanakimbia lakini ni zone Moja hii hii.
Asante
Mkuu kwanza pole kwa changamoto unayopitia na changamoto ndio mwalimu Mzuri katika kila kitu, kabla hujakimbilia kuanza kuongeza wingi wa chakula au kubadirisha aina ya chakula hebu tujaribu kujiuliza baadhi ya maswali ambayo yanaweza yakawa key factor katika kufanya maamuzi Yako hapo badae
Tuje kwenye mada sasa, unachotakiwa kujua ni kwamba kila kiumbe kitakuwa kulingana na wazazi wake au na mara chache ukoo wake, usitegemee baba ni mfupi na mama mfupi alafu upate watoto warefu ni ngumu sana unless otherwise Mke achepuke na mtu mrefu au labda babu au bibi aliwahi kuwa Tall
Kuhusu case Yako wewe kabla ya kuja kuomba ushauri wa nini ufanye ilitakiwa uwe ushajua tatizo nini, je we unawaona wanakua Kwa rate ndogo ukiwa unawafananisha na nguruwe wengine wepi? Je maumbo ya wazazi wao yakoje? Je ni nguruwe wa kisasa au kienyeji?
Ukijiuliza hayo maswali na majibu either yakawa, wazazi wao ni wenye maumbo makubwa swali lingine linakuja je ni kweli una uhakika ni wazazi wao? Maana muuzaji anaweza kudanganya akasema hawa wazazi wake ni yule na yule ila hakuna uhakika wowote hivo inabidi uwe umewatoa kwenye source inayoaminika
Jibu lingine ikawa ni nguruwe wa kisasa na sio kienyeji, ok swali lingine linakuja sawa ni nguruwe wa kisasa je ni pure kiasi gani? na wazazi wao walikuwa ni kabila Gani na wao ni pure kiasi gani, maana unaweza Kuta nguruwe ana historia tu ya kuwa wa kisasa ila hana tena ubora aliokuwa nao Babu yao kutokana na kuzaliana hovyo bila mpangilio
Linakuja swala la chakula, mkuu mind you kuwa nguruwe wa kisasa wanakula chakula kiasi kidogo sana ila output yao ni kubwa, na nguruwe wa kiswahili/kienyeji wanakula chakula kingi sana ila output yao ni ndogo sana, kwahiyo kama una nguruwe wa kisasa ili upate matokeo mazuri zaidi Siri Sio kulisha chakula kingi bari kurisha chakula kidogo chenye ubora (balance diet)
Mwisho wa siku unapoamua kufuga nguruwe jaribu kuwa makini sana kwenye aina ya nguruwe unaonunua kulingana na aina ya mradi wako, unaweza kununua nguruwe Kwa ajili ya kuuza Nyama ila wakawa na ukuaji mdogo sana hivo utapata hasara maana itabidi uwalishe Kwa muda mrefu sana ili angalau wafike au wakaribie uzito wa kuchinja uliokuwa umepanga