Mimi ni raia wa Tanzania kwa Kuzaliwa, nimekuwa na safari ndefu ya kutafuta maisha, bado sijafanikiwa sana lakini kidogo hivyohivyo. Nimefungua shamba la mifugo ambalo kidogo lipo porini. Kidogo naona usalama si mzuri kwani siku hizi mnaweza kutekwa na kufanywa chochote. Ndio nawaza walau niwe na silaha ya kujilinda tu. Je nifuate utaratibu gani ili nimiliki kihalali?