Msaada: Ni kweli Dar Es Salaam ipo Zanzibar?

Msaada: Ni kweli Dar Es Salaam ipo Zanzibar?

Dik

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
1,205
Reaction score
416
Heshima kwenu wana Jf,

Kuna jambo linatatiza sana hapa kijiweni kuhusu muungano wetu.Kuna jamaa ka rise mada hapa kwamba sababu kubwa ya CCM na Serikali kung'ng'ania muungano ni kwamba kwa mujibu wa ramani ya enzi za mkoloni mipaka ya Zanzibar inaonesha Dar es salaam kuwapo ndani yake.

Tumebishana sana na nikakumbuka Jf kwamba kuna watu wenye busara nyingi,hali kadhalika uelewa mkubwa.Naombeni msaada juu ya hili ndugu zanguni.

Mod naomba uzi huu upate nafasi japo nifumbuke akili.asanteni
 
mikoa ya tanganyika iko mingap.? ukifanikiwa kuifahamu hiyo mikoa bas nadhan unaweza kuanza kupata muafaka kidogo mkuu.
 
Dik,

..ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki ulikuwa eneo la miliki ya Sultani wa Znz.

..baadaye in the 1800s Sultani wa Zanzibar aliliuza eneo hilo kwa wakoloni wa Kijerumani.

..
 
Last edited by a moderator:
mkuu ni kweli kabisa, ndo mana mimi nataka Zanzibar ipate mamlaka kabili ili biashara ya Urojo na Kacholi ipambe moto dar es salaam. Yani sasa ivi mtu ukitaka urojo wa kununua ukiwa dar es salaam mpaka uende mji mkongwe Zanzibar, mambo gani haya sasa.

Acha katiba mpya iturahisishie mambo
 
Heshima kwenu wana Jf,

Kuna jambo linatatiza sana hapa kijiweni kuhusu muungano wetu.Kuna jamaa ka rise mada hapa kwamba sababu kubwa ya CCM na Serikali kung'ng'ania muungano ni kwamba kwa mujibu wa ramani ya enzi za mkoloni mipaka ya Zanzibar inaonesha Dar es salaam kuwapo ndani yake.

Tumebishana sana na nikakumbuka Jf kwamba kuna watu wenye busara nyingi,hali kadhalika uelewa mkubwa.Naombeni msaada juu ya hili ndugu zanguni.

Mod naomba uzi huu upate nafasi japo nifumbuke akili.asanteni

Tanganyika ilipopata UHURU ,Dar Es Salam ,Tanga,na Mtwara ilikuwa bado?Je Uhuru wa Zanzibar ulipatikana mwaka gani?Je,na Uhuru wa Mombasa,Msumbiji?

Ukiweza kung'amua hivi vidogo utajua kuwa hakuna ukweli kwenye hayo anayoyasema.Zanzibar ni Pemba na Unguja tu.
 
Umeshajiuliza Rwanda na Burundi??
Mipaka uheshimiwa.....
 
Mahesabu, Dik,

..Sultani alihamia Zanzibar toka Oman.

..makao makuu ya usultani yakawa ni Zanzibar.

..sasa sijui kwanini Zanzibar hawadai kwamba warejeshewe Oman yao.

..actually, Mombasa ilikuwa miliki ya Sultani wa Znz mpaka wakati Kenya inakaribia kupata uhuru.

..mimi nilitegemea Znz wangelidai eneo hilo[mombasa] kuliko hili la ukanda wa pwani ya Tanganyika ambalo inaeleweka kabisa kwamba Sultani alilipiga bei kwa Wajerumani.

..Lakini siwalaumu wa-Znz kwa kuwa na mawazo ya kujitwalia ukanda wa pwani toka kwa Watanganyika. Tumewazoesha vibaya kwa kuwakubalia kila jambo wanalodai ktk muungano wetu.

cc Ngondombole
 
Last edited by a moderator:
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao
 
Dar jana niliikuta kenya sijui kwa sasa ipo wapi maana inahama hama
 
Dik,

..ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki ulikuwa eneo la miliki ya Sultani wa Znz.

..baadaye in the 1800s Sultani wa Zanzibar aliliuza eneo hilo kwa wakoloni wa Kijerumani.

..

kwa hivyo mkataba wa kuuziana una nulify mipaka ya mwanzo?ni sawa na kusema kama muungano ukivunjika itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Tanganyika ilipopata UHURU ,Dar Es Salam ,Tanga,na Mtwara ilikuwa bado?Je Uhuru wa Zanzibar ulipatikana mwaka gani?Je,na Uhuru wa Mombasa,Msumbiji?

Ukiweza kung'amua hivi vidogo utajua kuwa hakuna ukweli kwenye hayo anayoyasema.Zanzibar ni Pemba na Unguja tu.

duh,maswali mazuri sana haya.sasa wanachong'ang'nia ni kitu gani?
 
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao

mkuu unaweza japo kututhibitishia kidogo?kuna maswali yameulizwa,nami nalazimika kukuuliza je
mikoa ya ukanda wa pwani yalikuwa bado yanatawaliwa pindi tanganyika imejipatia uhuru?
 
kwa hivyo mkataba wa kuuziana una nulify mipaka ya mwanzo?ni sawa na kusema kama muungano ukivunjika itakuwaje?

..YES, Sultani wa Znz aliuza eneo alilokuwa na "mamlaka" nalo na kitendo hicho kikabadilisha mipaka ya koloni la Wajerumani Afrika Mashariki.

..Muungano ukivunjika tutarudi kwenye mipaka iliyokuwepo mwaka 1964. Mipaka hiyo inahusisha eneo alilouza Sultani kuwa upande wa Tanganyika.
 
Mkuu unamawazo mazuri sana na unaonekana we ni mtu ya busara lakni mkuu hlojina ananiogopesha mimi unajua mimi anaogopaga majoka.Thatha mkuu wewe anaonaje ukabadili hyo jina? ili mimi asiendelee kukuogopa? nimtazamo2 mkuu.
 
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao
we ndo CHIZI kweli
 
Mimi ninachojua Delmitation treaty ya :1886 ilitambua kuwa maeneo ya pwani yote usawa wa maili 10 kuelekea bara kuanzia Tanga mpaka kaskazini ya mto Ruvuma ni ikiwepo DSM ni mali ya sultan wa Zanzibar. Mjerumani aliruhuhusiwa kuwa na whalehouse(godown)pale bandari ya DSM. Mkataba wa Heligoland wa 1890 mjerumani alipewa maeneo yote pwani za Tanganyika ikiwepo DSM sultan alilazimishwa na waingereza kukabidhi kwa fidia ya dola 2000. Hivyo Dar si Zanzibar. Mombasa pia haikuwa sehemu ya sultan bali waasi wa sultan waitwao Mazrui. MWALIMU NAWASILISHA.
 
asante sana kwa ufafanuzi....
 
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao

we marikiti ya wapi mkunazini au kwerekwe?? hiyo historia unayoijua wewe ya nyanya na vitunguu.eti itabidi zirudi Zanzibar...usipoangalia hata chombe itavutwa Tanganyika
 
agenda kuu mbili zilizofikiwa na OAU wakati inaanzishwa mojawapo ni kutambua mipaka iliyowekwa na serikali za kikoloni since kabla ya wao kuja tabora ya nyamwezi na wahehe wa iringa walijiona tofauti kabisa.hili lilifikiwa ili kuepusha Uganda kuidai kagera kwa kuwa lumanyisa anafanana na muta wa kampala na wamsumbiji wasiidai mtwara kwakuwa wote wanajichanja usoni.

Tanganyika ilitawaliwa na mjerumani huku Zanzibar ikiwa inaongozwa na sultan.sultan mara nyingi haandikwi kama mkoloni bali anaonekana kama mwenye kila haki juu ya Zanzibar.wajerumani na sultan walitawala maeneo yenye kutegemeana kwa kiasi kikubwa,kisiwa na bara.sultan alitaka sana mamlaka juu ya maswala ya bahari.alipata urahisi wa kusafirisha watumwa,bidhaa na vile vile alipata kodi kwa kila meli iliyotia nanga.

baada ya kuja kwa mjerumani mwaka 1885 kutawala rasmi Tanganyika walikuta sultan anamiliki eneo ndani ya koloni lao.ikawabidi wakutane ili wawekeane ukomo wa madaraka juu ya mgongo wa ardhi.hivyo 1886 walikutana na sultani akaachiwa 10 kms kwenye ukanda wa bahari(mikutano hii iliihusisha na uingereza).bado hii ilimpa sultan nguvu ya kumiliki bandari ambayo ni muhimu kwa kila koloni.huo ndio mkataba wa kwanza kuwekwa.

ni wazi makubaliano yao hayakuwa sahihi.baadhi ya maeneo ikiwemo hizo 10 kms ziliacha migogoro.ujerumani asingeweza kulipa kodi miaka yote.hivyo mwaka 1890 walikutana tena na Zanzibar akalitoa eneo hili kwa makubaliano yakwao wenyewe.alipoteza authority juu ya eneo hili.

mkataba huu wa 1890 ndio wa mwisho kabisa kuwekwa hivyo kwa makubaliano ya OAU yaliyotajwa hapo juu ukanda huu ni mali ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom