Heshima kwenu wana Jf,
Kuna jambo linatatiza sana hapa kijiweni kuhusu muungano wetu.Kuna jamaa ka rise mada hapa kwamba sababu kubwa ya CCM na Serikali kung'ng'ania muungano ni kwamba kwa mujibu wa ramani ya enzi za mkoloni mipaka ya Zanzibar inaonesha Dar es salaam kuwapo ndani yake.
Tumebishana sana na nikakumbuka Jf kwamba kuna watu wenye busara nyingi,hali kadhalika uelewa mkubwa.Naombeni msaada juu ya hili ndugu zanguni.
Mod naomba uzi huu upate nafasi japo nifumbuke akili.asanteni
Dik,
..ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki ulikuwa eneo la miliki ya Sultani wa Znz.
..baadaye in the 1800s Sultani wa Zanzibar aliliuza eneo hilo kwa wakoloni wa Kijerumani.
..
Tanganyika ilipopata UHURU ,Dar Es Salam ,Tanga,na Mtwara ilikuwa bado?Je Uhuru wa Zanzibar ulipatikana mwaka gani?Je,na Uhuru wa Mombasa,Msumbiji?
Ukiweza kung'amua hivi vidogo utajua kuwa hakuna ukweli kwenye hayo anayoyasema.Zanzibar ni Pemba na Unguja tu.
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao
Dar jana niliikuta kenya sijui kwa sasa ipo wapi maana inahama hama
kwa hivyo mkataba wa kuuziana una nulify mipaka ya mwanzo?ni sawa na kusema kama muungano ukivunjika itakuwaje?
..YES, Sultani wa Znz aliuza eneo alilokuwa na "mamlaka" nalo na kitendo hicho kikabadilisha mipaka ya koloni la Wajerumani Afrika Mashariki.
..Muungano ukivunjika tutarudi kwenye mipaka iliyokuwepo mwaka 1964. Mipaka hiyo inahusisha eneo alilouza Sultani kuwa upande wa Tanganyika.
we ndo CHIZI kweliKumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao
asante sana kwa ufafanuzi....Mimi ninachojua Delmitation treaty ya :1886 ilitambua kuwa maeneo ya pwani yote usawa wa maili 10 kuelekea bara kuanzia Tanga mpaka kaskazini ya mto Ruvuma ni ikiwepo DSM ni mali ya sultan wa Zanzibar. Mjerumani aliruhuhusiwa kuwa na whalehouse(godown)pale bandari ya DSM. Mkataba wa Heligoland wa 1890 mjerumani alipewa maeneo yote pwani za Tanganyika ikiwepo DSM sultan alilazimishwa na waingereza kukabidhi kwa fidia ya dola 2000. Hivyo Dar si Zanzibar. Mombasa pia haikuwa sehemu ya sultan bali waasi wa sultan waitwao Mazrui. MWALIMU NAWASILISHA.
Kumbe mijitu mingine inabishana tu lakini haijui historia sikiliza tanga dsm pwani lindi mtwara zipo zanzibar muungano ukifa inabidi zirudi zannzibar au ziunde nchi yao