Nifumbue macho zaidi
Sent using
Jamii Forums mobile app
kabla ya kununua ni vizuri kufanya 'official search' katika ofisi ya ardhi hapo arusha na jiridhishe katika haya:
1. jina la muuzaji liwe sawa na jina la mmiliki kama ulivyoona kutoka ofisi ya ardhi.
2. kuwajua majirani wanaopakana na nyumba/ardhi unayotaka inunua.
3. kushirikisha mwanasheria/mahakama wakati wa kufanya makubaliano/malipo.
4. hakikisha unafanya malipo kupitia akaunti ya benki inayomilikiwa na muuzaji ikiwezekana ulipe kwa instalments japo mbili.
5. hakikisha kuna mashahidi wa muuzaji/mnunuzi wanakuwepo wakati wa makubaliano ikiwezekana na muda unaofanya malipo.
6. hakikisha kuna mkataba wa makubaliano ya kuuziana nyumba utakaokuwa na sahihi za muuzaji,mnunuzi pamoja na mashahidi.
7. hakikisha mnakamilisha mauziano kwa kujaza na kusaini 'land form no. 35' ya "transfer of a right of occupancy" iliyoko kwenye Act No. 15 of 1999 under Section 62.
8. hakikisha mnakamilisha mauziano kwa kujaza na kusaini 'land form no. 38' ya "contract for a disposition of a right of occupancy " iliyoko kwenye Act No. 15 of 1999 under Section 62.
9. hakikisha mnakamilisha mauziano kwa kujaza na kusaini 'land form no. 29 ' ya "notification of a disposition" iliyoko kwenye Act No. 15 of 1999 under Section 36.
10. hakikisha mnakamilisha mauziano kwa kujaza na kusaini 'land form no. 30' ya "application for approval of disposition" iliyoko kwenye Act No 15 of 1999 under Section 39.
11. hakikisha mnakamilisha mauziano kwa kujazwa na kusainiwa kwa 'consent by spouse to disposition of a right of occupancy' iliyoko kwenye Act No. 4 of 1999.
12. hakikisha unajaza na kusaini 'commitment bond' iliyoko kwenye Act No. 4 of 1999.
13. hakikisha kodi zote za ardhi/jengo zimelipwa mpaka wakati wa kufanya mauziano.
note: sina taaluma wala ujuzi wa sheria ila hizi ni hatua ambazo niliwahi pitia nilipofanya mauziano/manunuzi ya ardhi/nyumba kwa hiyo marekebisho yanaruhusiwa.